Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
إِذْ قَالَ ٱللَّهُ يَـٰعِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ ٱذْكُرْ نِعْمَتِى عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَٰلِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ ٱلْقُدُسِ تُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِى ٱلْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ ٱلطِّينِ كَهَيْـَٔةِ ٱلطَّيْرِ بِإِذْنِى فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًۢا بِإِذْنِى ۖ وَتُبْرِئُ ٱلْأَكْمَهَ وَٱلْأَبْرَصَ بِإِذْنِى ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ ٱلْمَوْتَىٰ بِإِذْنِى ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ۱۱۰
{110} "Na pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako;" yaani, ikumbuke kwa moyo wako na ulimi wako, na ufanye wajibu wake kwa kumshukuru Mola wako Mlezi. Kwani alikuneemesha neema ambazo hakumneemesha kwazo mwengine yeyote, "nilipokutia nguvu kwa Roho Mtakatifu; yaani, nilipokutia nguvu kwa Roho na wahyi ambao ulitasafisha na kukutakasa na ukapata nguvu za kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kulingania kwenye njia yake. Na ilisemwa: Maana ya Roho Mtakatifu ni Jibril, amani iwe juu yake, na kwamba Mwenyezi Mungu alimsaidia kupitia kwake na kwa kuandamana naye na kumtia nguvu katika sehemu za shida, "ukazungumza na watu katika utoto na utu uzimani." Kinachomaanishwa na kuzungumza hapa siyo kuzungumza kwa kawaida ambako maneno tu, bali kile kinachomaanishwa na kuzungumza ambako ananufaika nako mzungumzaji na anayezungumzishwa. Nako ni kulingania kwa Mwenyezi Mungu. Na Isa, amani iwe juu yake alikuwa na uwezo sawa na ule wa ndugu zake miongoni mwa Mitume wenye stahamala kubwa zaidi, katika kuzungumza ujumbe wakati wa utu uzima wake na kulingania kheri na kukataza maovu, lakini yeye Isa alijipambanua nao kwa kuzungumza na watu katika utoto. Alisema, "Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai..." hadi mwisho wa Aya. "Na nilivyokufunza kuandika na hekima." Na maana ya Kitabu hapa inajumuisha vitabu vilivyotangulia, hasa Taurati. Kwani yeye ndiye mwenye elimu zaidi juu yake miongoni mwa Manabii wa Wana wa Israili baada ya Musa. Na inajumuisha Injili ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia. Nayo Hekima ni kujua siri za Sheria, na faida zake na hekima zake, na kulingania kuzuri na kufundisha, na kuzingatia yale yanayofaa kwa namna ifaayo. "Na ulipotengeneza udongo umbo la ndege; yaani, ndege mwenye umbo ambaye hana roho ndani yake. "Kisha unapuliza" ndani yake (umbo hilo) na linakuwa "ndege" kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; "ulipowaponya vipofu," ambaye haoni wala hana macho, "na wakoma kwa idhini yangu; na ulipowafufua wafu kwa idhini yangu." Basi Aya hizi zilizo wazi na miujiza ya kung'aa ambayo madaktari na wengineo hawaiwezi, Mwenyezi Mungu alimuunga kwayo mkono Isa na akaupa kwayo nguvu ulinganizi wake. "Na nilipokukinga na Wana wa Israili ulipowajia na hoja zilizo wazi, na wakasema wale waliokufuru miongoni mwao," ilipowajia haki iliyoungwa mkono na hoja zilizo wazi zinazolazimu kuiamini. "Haya si lolote isipokuwa uchawi ulio wazi" na wakaazimia kumuua Isa, na wakafanya juhudi kubwa katika hilo, lakini Mwenyezi Mungu akaizuia mikono yao dhidi yake, na akamhifadhi kutokana nao, na akamlinda. Basi hizi ni neema alizomneemesha kwazo Mwenyezi Mungu mja wake na Mtume wake Isa bin Maryamu na akamwita kuzishukuru na kuzitekeleza. Kwa hivyo akazifanya, yeye amani iwe juu yake, kufanya kukamilifu, na akawa na subira kama walivyosubiri ndugu zake miongoni mwa wenye stahamala kubwa.