Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ شَهَـٰدَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ حِينَ ٱلْوَصِيَّةِ ٱثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ ءَاخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَأَصَـٰبَتْكُم مُّصِيبَةُ ٱلْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِنۢ بَعْدِ ٱلصَّلَوٰةِ فَيُقْسِمَانِ بِٱللَّهِ إِنِ ٱرْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِى بِهِۦ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَـٰدَةَ ٱللَّهِ إِنَّآ إِذًا لَّمِنَ ٱلْـَٔاثِمِينَ ۱۰۶
{106} Yeye Mtukufu anajulisha habari inayojumuisha amri ya kuwashuhudisha wawili juu ya wasia, ikiwa mtu anafikiwa na vitangulizi vya kifo na dalili zake. Basi inamfaa aandike wasia wake, na awashuhudishe juu yake watu wawili waadilifu ambao ushahidi wao unachukuliwa. "Au wengineo wawili wasiokuwa katika nyinyi," yaani, kutoka kwa watu wasiokuwa wa Dini yenu kama vile Mayahudi, na Wakristo, au wengineo. Na hilo ni panapokuwa na haja na dharura, na kutokuwepo kwa wasiokuwa wao miongoni mwa Waislamu; "Mnapokuwa katika safari na msiba wa mauti ukawasibu; yaani, washuhudisheni wawili hao. Na hakuamrisha kuwashuhudisha wawili hao isipokuwa kwamba maneno yao katika hali hiyo yanakubalika, na unasisitizwa ushahidi huo kuwa wazuiliwe "baada ya Swala;" ambayo wanaitukuza. "Na waape kwa Mwenyezi Mungu" ya kwamba wamesema kweli, wala hawakughairi, wala hawakulibadilisha hili, "mkitilia shaka;" katika ushahidi wao. Kwa hivyo wakiwasadiki, basi hakuna haja ya kuapa kwa hilo. Na waseme: "Hatutopokea kwa haya;" yaani, kwa viapo vyetu, "thamani yoyote" kwa kusema uongo katika hili kwa ajili ya manufaa ya kidunia, "hata kama ni jamaa." Kwa hivyo hatutamlalia kwa sababu ya ukaribu wake kwetu, "na wala hatutauficha ushahidi wa Mwenyezi Mungu;" bali tutautekeleza kama tulivyousikia. Yaani, "hakika hapo," ikiwa tutaficha "tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi."