Al-Jaathiya
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً ۚ كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰٓ إِلَىٰ كِتَـٰبِهَا ٱلْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ۲۸
{28} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza ukali na mahangaiko ya Siku ya Kiyama ili waja wajihadhari nayo na wajiandae kwa ajili yake. Akasema: "Na utauona" ewe mwenye kuona siku hiyo, "kila umma umepiga magoti" kwa hofu, kufadhaika na kungojea hukumu ya Mfalme, Mwingi wa rehema. "Kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake." Yaani, kwenye sheria ya Mtume wao aliyewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na je waliitekeleza; ili wapate malipo mazuri na wokovu? Au waliipoteza; kwa hivyo wapate hasara? Basi umma wa Musa wataitwa kwenye sheria ya Musa, na umma wa Isa utaitwa vivyo hivyo, na umma wa Muhammad utaitwa vivyo hivyo, na wengineo vile vile. Kila umma utaitwa kwenye sheria yake ambayo ulijukumishwa.' Huu ni uwezekano mmoja wa maana za Aya hii, nao ndio wenye maana sahihi yenyewe, usio na shaka yoyote. Na inawezekana kwamba kile kinachokusudiwa na kauli yake: "Na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake," ni kitabu cha matendo yake waliyoandikiwa; mema na mabaya, na kwamba kila mtu atalipwa kwa aliyoyafanya yeye mwenyewe. Kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Anayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile." Na inawezekana kwamba maana zote mbili zimekusudiwa na Aya hii.