Al-Ghaafir
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِىَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ فَإِذَا جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ قُضِىَ بِٱلْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلْمُبْطِلُونَ ۷۸
Kisha akamliwaza, akamfanya kuwa na subira kwa kuwataja ndugu zake Mitume, akasema:
{78} Yaani, "bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako" kwenda kwa kaumu zao wakiwalingania na wakawa na subira kwa maudhi yao. "Wengine katika hao tumekusimulia habari zao na wengine hatukukusimulia." Na Mitume wote wanaendeshwa na Mwenyezi Mungu, wala hawana uwezo wowote juu ya jambo hili. "Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote" miongoni mwa ishara za kusikika na za kiakili "ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, mapendekezo ya wenye kuwapendekezea Mitume wao kuwaletea ishara fulani ni dhuluma kwa upande wao, ukaidi na kukadhibisha baada ya Mwenyezi Mungu kuwaunga mkono kwa ishara zinazoonyesha ukweli wao na usahihi wa yale waliyokuja nayo. "Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu" ili kukata hukumu kati ya Mitume na maadui zao na ushindi, "huhukumiwa kwa Haki" inayoanguka mahali pake na kuafikiana na usahihi kwa kuwaokoa Mitume hao na wafuasi wao na kuwaangamiza wale waliokadhibisha. Ndiyo maana akasema: "na hapo watahasiri wana batili" ambao wanasifika kwa batili na hata waliyoyaleta katika elimu, na matendo yote pia ni batili, na lengo lao wanalokusudia ni batili. Basi hao wanaoongeleshwa na wajihadhari wasije wakaendelea na batili yao, wakaja kuhasiri kama walivyohasiri wenzao. Kwani watu hawa si bora kuliko wao na hawakuandikiwa vitabuni kuwa wataokolewa