Al-Ghaafir
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱللَّهُ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ قَرَارًا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ۶۴
{64} "Ni Mwenyezi Mungu aliyewafanyia ardhi kuwa ni pahala pa kukaa," ikawa imeandaliwa kwa ajili ya masilahi yenu yote ambayo mnaweza kuilima, kuipanda, kujenga juu yake, kusafiri na kukaa juu yake, "na mbingu kuwa dari" ya ardhi ambayo mko ndani yake. Mwenyezi Mungu ameweka humo mambo ya kuwanufaisha kama vile nuru na alama mbalimbali, Ishara zinazowaongoza katika kiza cha bara na bahari. "Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu." Hakuna mnyama mwenye sura nzuri zaidi kuliko wanadamu. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lililo bora kabisa." Na ukitaka kujua uzuri wa mwanadamu na ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu kuhusiana naye, basi mtazame kiungo kwa kiungo. Je, unapata kiungo chochote kinachomfailia na kinachofaa kuwa katika mahali ambapo si pake? Pia tazama namna ulivyo mwelekeo uliomo mioyoni mwao wa mtu kwa mwengine. Je, unayapata hayo kwa wasiokuwa wanadamu? Na angalia kile ambacho Mwenyezi Mungu amempa yeye tu ambacho ni akili, imani, upendo na kujua, ambayo ndiyo maadili bora zaidi yanayolingana na sura nzuri zaidi. "Na akakuruzukuni vitu vizuri" miongoni mwa vyakula, vinywaji, ndoa, mavazi, uwezo wa kuona, kusikia na mengineyo miongoni mwa mambo mazuri ambayo Mwenyezi Mungu amewafanyia wepesi waja wake. Akawafanyia wepesi visababu vyake na akawazuia mbali na mambo maovu yanayopingana na hayo na kuwadhuru miili yao, nyoyo zao na dini zao. "Huyo" aliyepanga mambo na akakuneemesheni neema hizi, "ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote." Yaani, heri yake na wema wake ni kubwa na nyingi, naye ndiye anayewalea walimwengu wote kwa neema zake.