An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذَا جَآءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ ٱلْأَمْنِ أَوِ ٱلْخَوْفِ أَذَاعُوا۟ بِهِۦ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُو۟لِى ٱلْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسْتَنۢبِطُونَهُۥ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ لَٱتَّبَعْتُمُ ٱلشَّيْطَـٰنَ إِلَّا قَلِيلًا ۸۳
{83} Huku ni kufundisha adabu kutokako kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa kitendo chao hiki kisichofaa. Na kwamba inawapasa wanapojiwa na jambo katika mambo muhimu na masilahi ya umma yanayohusiana na usalama na furaha ya Waumini, au ya hofu ambayo ndani yake kuna msiba juu yao kwamba wawe wadhibitishe na wala wasiharakishe kueneza habari hizo. Bali wazirudishe kwa Mtume na kwa wenye mamlaka miongoni mwao, wenye maoni, na elimu, na ushauri, na akili, na utimamu, ambao wanajua mambo na wanajua masilahi na kinyume chake. Na wakiona masilahi katika kuyatangaza na ukakamavu kwa Waumini na furaha kwao, na ulinzi dhidi ya maadui zao, basi wanafanya hivyo. Na wakiona [kwamba hakuna] masilahi ndani yake, au kuna masilahi ndani yake, lakini madhara yake yanazidi masilahi yake, hawayatangazi. Ndiyo maana akasema, “wale wanaochunguza miongoni mwao wangelilijua,”yani wanayatoa kwa fikira zao, na rai zao zilizo sawasawa, na elimu zao zilizoongoka. Na katika hili kuna ushahidi wa msingi wa kiadabu, nao ni kwamba ikiwa kuna utafiti katika jambo miongoni mwa mambo, basi inapasa apewe hilo yule ambaye anafaa zaidi kufanya hivyo,. Na lipewe kwa wale wanaolistahiki, na wala asitangulizwe yeyote mbele yao. Kwa sababu hili liko karibu zaidi na usahihi na lenye uwezekano mkubwa wa kuwa salama kuliko makosa. Na ndani yake kuna katazo dhidi ya kufanya pupa, na kuharakisha katika kueneza mambo tangu yanaposikika, na amri ya kutafakari kabla ya kusema, na kulizingatia, je ni masilahi ili mtu ayaendee, au hapana ili ajizuie kuyaendea? Kisha Yeye Mtukufu akasema, "Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake." Yani katika kuwawezesha, na kuwaadibu, na kuwafundisha yale ambayo hamkuwa mkiyajua. "Basi mngelimfuata Shetani isipokuwa wachache tu." Kwa sababu, mwanadamu kulingana na umbile lake la asili ni dhalimu, mjinga. Kwa hivyo, nafsi yake haimwamrishi isipokuwa maovu. Lakini, akimkimbilia Mola wake Mlezi, na akashikamana naye, na akajitahidi katika hayo, Mola wake Mlezi anamfanyia upole, na anamwezesha kila la heri, na anamlinda kutokana na Shetani aliyelaaniwa.