An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا۟ مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ ٱلَّذِى تَقُولُ ۖ وَٱللَّهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا ۸۱
{81} Na ni lazima utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwe kwa dhahiri na kwa ndani, mbele ya watu na kwa ghaibu. Ama yule anayeonyesha utiifu na kushikamana na sheria mbele ya watu, na anapokuwa peke yake au pamoja na watu wa mfano wake, anaacha utiifu na anaelekea kinyume chake. Kwani, utiifu ule alioudhihirisha haunufaishi wala haufai, na amefanana na wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao, “Na wanasema: Tunatii” Yani wanaonyesha utiifu wanapokuwa pamoja nawe. “Lakini wanapotoka kule uliko” Yani wanapotoka na wakabaki peke yao katika hali ambayo hawaonekani, “kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayoyasema.” Yani wanakaa usiku, na wanapanga yasiyokuwa kukutii, na kisha hakuna hapo isipokuwa kukuasi. Na katika kauli yake, “kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayoyasema;” kuna ushahidi wa kuwa jambo walilokubaliana juu yake si utiifu, kwa sababu Tabyit ni kupanga jambo usiku kwa namna ambayo hiyo ndiyo inakuwa rai iliyokubaliwa juu yake. Kisha akawaahidi adhabu kwa yale waliyoyatenda, akasema, “Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayoyapangia njama za usiku.” Yani atawahifadhia na atawalipa juu yake malipo kamili. Kwa hivyo, ndani yake kuna ahadi ya adhabu kwao. Kisha akamuamuru Mtume wake awakabili kwa kuwapa mgongo, na kutokuwa mkali. Kwa maana, wao hawatomdhuru kitu ikiwa atamtegemea Mwenyezi Mungu, na akamwomba msaada katika kuinusuru Dini yake na kuisimamisha sheria yake. Na ndiyo maana akasema, “Basi wape mgongo, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.”