An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱلطَّـٰغُوتِ فَقَـٰتِلُوٓا۟ أَوْلِيَآءَ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۖ إِنَّ كَيْدَ ٱلشَّيْطَـٰنِ كَانَ ضَعِيفًا ۷۶
Kisha akasema:
{76} Huku ni kujulisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba Waumini wanapigana katika Njia yake, “na wale waliokufuru wanapigana vita katika njia ya Twaghut” ambaye ni Shetani. Na ndani yake kuna faida kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba kulingana na imani ya mja, inakuwa jihadi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ikhlasi yake, na kufuata kwake. Kwa hivyo, Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni katika athari za imani, na matakwa yake, na yale yanyolazimiana nayo, kama vile kupigana vita katika njia ya Twaghut (Shetani) ni katika matawi ya ukafiri na matakwa yake. Na miongoni mwake ni kwamba yule ambaye anapigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu anapaswa na ni bora kwake kuwa na subira na stahamala ambayo haiwi kwa asiyekuwa yeye. Basi, ikiwa marafiki wa Shetani wanasubiri na wanapigana vita ilhali wako katika batili, basi watu wa haki wanastahiki zaidi hayo, kama alivyosema Yeye Mtukufu katika maana hii. “Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyataraji wao.” Hadi mwisho wa Aya. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kupigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu akitegemea kwenye nguzo madhubuti, ambayo ni haki na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, mwenye nguvu na nguzo madhubuti anatakiwa kuwa na subira, na uthabiti, na ukakamavu ambao haitakiwi kwa yule anayepigana vita kwa sababu ya batili ambayo haina uhakika wala mwisho wenye kusifiwa. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, “Basi piganeni na marafiki wa Shetani. Hakika, hila ya Shetani ni dhaifu.” Na hila ni kutumia njia zilizofichika ili kumdhuru adui. Kwa hivyo, Shetani, hata kama vitimbi vyake vitafikia kiwango vitakachofikia, yeye kwa hakika ni dhaifu sana na haiwezi kustahimili haki ya chini kabisa, wala vitimbi vya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake Waumini.