An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا۟ ٱلْأَمَـٰنَـٰتِ إِلَىٰٓ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ ٱلنَّاسِ أَن تَحْكُمُوا۟ بِٱلْعَدْلِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ سَمِيعًۢا بَصِيرًا ۵۸
{58} Amana ni kila alichokabidhiwa mtu na kuamrishwa kukisimamia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake wavirudishe vikiwa kamili, vingi, bila ya kupunguzwa, wala kupunjwa, wala kucheleweshwa. Na inaingia katika hilo amana walizopewa walezi, na mali, na siri, na maamrisho ambayo hawezi kuyajua isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeweza. Na wanachuoni wa Fiqh walisema kwamba mwenye kukabidhiwa amana, inamlazimu aihifadhi katika pahali salama pa kitu mfano wake. Walisema, "Kwa sababu haiwezekani kuirudisha isipokuwa kwa kuihifadhi, kwa hivyo hilo likawa ni wajibu." Na katika kauli yake, "kwa wenyewe" kuna ushahidi kuwa haipeanwi na kurudishwa kwa asiyekuwa aliyeipeana kama amana, na wakili wake yuko katika nafasi yake. Basi ikiwa atairudisha kwa asiye mwenyewe, hapo hatakuwa ameirudisha. "Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu." Na hili linajumuisha kuhukumu baina yao katika damu, na mali, na heshima; kidogo katika hayo na kingi, kwa walio karibu na walio mbali, na mwema na muovu, na rafiki na adui. Na kinachokusudiwa na uadilifu alioamrisha Mwenyezi Mungu kuhukumu kwao ni yale aliyoyaweka Mwenyezi Mungu kama sheria kwa ulimi wa Mtume wake miongoni mwa adhabu maalum na hukumu. Na hili linalazimu kuujua uadilifu ili ahukumu kwayo. Na kwa kuwa haya ni maamrisho mazuri, ya uadilifu, akasema, "Hakika haya anayowawaidhi kwayo Mwenyezi Mungu ndiyo mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona." Na huku ni kusifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya amri zake na makatazo yake kwa sababu ya kujumuisha kwake masilahi ya Nyumba mbili hizi na kuzuia madhara yake. Kwa sababu mweka sheria hizo ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, hikifichiki kwake chenye kufichika, na anayejua katika masilahi ya waja yale wasiyoyajua.