پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورهٔ ۴

An-Nisaa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۳۶–۳۷

وَٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا۟ بِهِۦ شَيْـًٔا ۖ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَـٰنًا وَبِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱلْجَارِ ذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْجَارِ ٱلْجُنُبِ وَٱلصَّاحِبِ بِٱلْجَنۢبِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ۳۶ ٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ۳۷

{36-37} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake kumwabudu Yeye peke yake asiyekuwa na mshirika yeyote. Na hilo ni kuingia chini ya uja wa kumfanyia ibada, na kufuata maamrisho yake, na makatazo yake kwa upendo, na unyenyekevu, na kumfanyia yeye peke yake katika ibada zote za dhahiri na za ndani. Na anakataza kumshirikisha na chochote, si shirki ndogo wala shirki kubwa, wala Malaika, wala Nabii, wala mlinzi, wala asiyekuwa wao miongoni mwa viumbe ambao hawazimilikii nafsi zao manufaa wala madhara, wala mauti, wala uhai, wala kufufuka. Bali, wajibu wa pekee ni kumwabudu Yeye peke yake ambaye ana ukamilifu kamili kwa namna zote, na ana uendeshaji kamili ambao hashirikiani naye, wala hamsaidii yeyote kwa hilo. Kisha baada ya kuamrisha kumwabudu na kutekeleza haki zake, akaamrisha kutekeleza haki za waja wake, walio karibu zaidi kisha walio karibu zaidi. Akasema, “Na wafanyieni wema wazazi wawili” Yani wafanyieni wema kwa kusema maneno mazuri, maneno ya upole, na vitendo vizuri, kwa kutii amri zao na kuepuka makatazo yao, na kuwapa matumizi, na kumkirimu yeyote anayefungamana nao, na kuunga ukoo ambao hauna ukoo nao isipokuwa kupitia wao. Na wema una vinyume viwili: kutendewa ubaya na kutotenda wema, na vyote viwili vimekatazwa. “Na jamaa” pia wafanyiwe wema. Na hilo linajumuisha jamaa wote, walio karibu au walio mbali. Kwamba wafanyiwe wema kwa kauli na vitendo, na kwamba asiukate ukoo wake kwa maneno yake au vitendo vyake. “Na mayatima,” yani wale waliofiwa na baba zao hali ya kuwa ni wadogo. Basi wanayo haki juu ya Waislamu, sawa wawe ni jamaa au wasiokuwa wao, kwa kuwalea, na kuwafanyia wema, na kutuliza fikira zao, na kuwafunza adabu nzuri, na kuwalea kwa njia iliyo bora kabisa ya malezi katika masilahi ya dini yao na dunia yao. “Na masikini” na hao ndio waliotulizwa harakati zao mahitaji na ufukara, na hawawezi kupata cha kuwatosheleza wala cha kuwatosheleza wale ambao wao wanaowaruzuku. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha wafanyiwe wema kwa kuziba mapengo yao, na kuuzuia umaskini wao, na kuhimiza juu ya hilo, na kufanya kile kinachowezekana katika hayo. “Na jirani wa karibu,” yani jirani wa karibu ambaye ana haki mbili: Haki ya ujirani na haki ya ujamaa. Yeye ana haki juu ya jirani yake, na wema kulingana na desturi. Na vivyo hivyo “jirani wa mbali” yani ambaye hana ujamaa. Na kila anapokuwa jirani ana mlango ulio karibu zaidi nawe, anakuwa na haki inayosisitizwa zaidi. Kwa hivyo, jirani anapaswa amjulie hali mara kwa mara jirani yake kwa kumpa zawadi, na sadaka, na kumlingania, na upole katika maneno na vitendo, na kutomdhuru kwa maneno au vitendo. “Na mwenza wa ubavuni” inasemekana kuwa ni mwenza katika safari, na inasemekana kuwa ni mke, na inasemekana kuwa ni mwenza yeyote yule, na huenda hii maana ndiyo inafaa zaidi, kwa kuwa inajumuisha mwenza wakati usio wa safari na safarini, na inajumuisha mke. Basi mwenza ana haki ya ziada juu ya Uislamu wake tu kwa mwenza wake kama vile kumsaidia katika mambo ya dini yake na ya dunia yake, kumnasihi, kumtimizia ahadi katika wepesi na ugumu, na katika hali ya kusisimua na hali ya kuchukia, na kwamba anampendee kile anachoipendea nafsi yake, na amchukilie kile anachoichukia nafsi yake. Na wenza unavyoongezeka, haki inasisitizwa zaidi na inaongezeka. “Na mwana njia;” naye ni mgeni ambaye ana mahitaji katika nchi ya ugeni au hata ikiwa hana mahitaji. Basi yeye ana haki juu ya Waislamu kwa sababu ya uzito wa mahitaji yake na kwa kuwa yuko katika nchi isiyokuwa nchi yake, kwa kumfahamisha kwenye makusudio yake au baadhi ya makusudio yake, na kwa kumkirimu na kumfanya atulizane. “Na wale iliowamiliki mikono yenu ya kulia.” Yani katika binadamu na wanyama, kwa kuwafanyia yale yanayowatosheleza na kutowabebesha yaliyo magumu kwao, na kuwasaidia katika yale wanayoyabeba na kuwafunza adabu nzuri kwa yale yenye masilahi yao. Kwa hivyo, mwenye kutimiza amri hizi, basi yeye amenyenyekea kwa Mola wake Mlezi, amejishusha chini kwa waja wa Mwenyezi Mungu, ametii amri ya Mwenyezi Mungu na sheria yake, ambaye anastahiki thawabu nyingi na sifa nzuri. Na asiyefanya hivyo; yeye kwa hakika ni mja anayempa mgongo Mola wake Mlezi, asiyekuwa mtiifu kwa amri zake, wala asiyejishusha chini kwa viumbe. Bali, ana kiburi kwa waja wa Mwenyezi Mungu, anajiona nafsi yake, anajifahiri kwa maneno yake. Ndiyo maana akasema, “Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi mwenye kiburi;” yani anayejiona nafsi yake, mwenye kiburi juu ya viumbe. “Anayejifahiri” anayejisifu na kujihimidi kwa namna ya kujifahiri na kujigamba mbele ya waja wa Mwenyezi Mungu. Basi hawa, kwa sababu ya yale waliyo nayo ya kiburi na kujifahiri yanawazuia kutekeleza haki mbalimbali, na kwa sababu hiyo akawakashifu kwa kauli yake. “Ambao wanafanya ubahili,” yani wanazuilia yale yaliyo juu yao miongoni mwa haki za lazima. “Na wanaamrisha watu ubahili” kwa kauli zao na vitendo vyao, “na wanaficha yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake.” Yani elimu ambayo wanaongoka kwayo waliopotea, na wanaongozwa kwayo wasiojua. Hao wanawaficha hayo na wanawadhihirishia ubatili ambao unazuia kati yao na haki. Kwa hivyo wakawa wamekusanya kati ya kufanyia mali ubahili na kufanyia elimu ubahili, na baina ya kujitahidi katika kujihasiri na kuwahasirisha wengine. Na hizi ndizo sifa za makafiri. Ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, “Na tuliwaandalia makafiri adhabu ya kudunisha.” Yani kwa vile walivyokuwa wakijivuna mbele ya waja wa Mwenyezi Mungu, na wakazuia haki zake, na walikuwa ndiyo sababu ya wengine kuzuia na kufanya ubahili na kutoongoka, akawadunisha kwa adhabu chungu na hizaya ya daima. Kwa hivyo, tunajilinda kwako ewe Mwenyezi Mungu kutokana na mabaya yote.