An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى ٱللَّهِ حُجَّةٌۢ بَعْدَ ٱلرُّسُلِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ۱۶۵
{165} Na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatuma kuwaletea bishara njema - mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akawafuata - furaha ya kidunia na ya kiakhera, na kumuonya mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na kuwahalifu kwamba watapata taabu katika Nyumba hizi mbili; "ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume." Wakasema, 'hakutujia mbashiri yeyote wala mwonyaji.' Sema: 'Amekwisha wajia mbashiri na mwonyaji.' Basi hakuna hoja yoyote iliyobaki ya viumbe dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu aliwatuma mitume mmoja baada ya mmoja wakiwaelezea mambo ya dini yao, na radhi za Mola wao Mlezi, na ghadhabu zake, na njia za Pepo, na njia za Moto. Basi mwenye kukufuru miongoni mwao baada ya hayo, na asilaumu kabisa isipokuwa nafsi yake. Na hili ni katika ukamilifu wa nguvu zake Yeye Mtukufu na hekima yake. Na kwamba aliwatumia Mitume na akawateremshia vitabu, na hayo pia ni katika fadhila zake na wema wake. Kwa kuwa watu walikuwa wanawahitaji manabii vikubwa zaidi iwezekanavyo, kwa hivyo akaliondoa hitaji hilo. Basi ni zake Sifa njema na shukurani, na tunamuomba kama vile alivyoanzisha neema zake juu yetu kwa kuwatuma, kwamba aitimize juu yetu kwa kutuwezesha kufuata njia yao. Yeye hakika ndiye Mtoaji kwa wingi, Mkarimu.