An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ۱۵۱ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَلَمْ يُفَرِّقُوا۟ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُو۟لَـٰٓئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ۱۵۲
{151 - 152} Na kwa sababu ya hilo akasema, "Hao ndio makafiri wa hakika," na hilo ni kwa sababu ili isije ikadhaniwa kuwa cheo chao ni cha katikati ya Imani na ukafiri. Na sababu ya wao kuwa makafiri hata katika yale waliyodai kuwa wanayaamini; ni kwamba kila ushahidi uliowaelekeza kumwamini yule waliyemwamini ipo hiyo yenyewe, au mfano wake, au iliyo juu zaidi kuiliko kwa Nabii ambaye walimkufuru. Na kila dhana potofu wanayodai kumkashifu kwa nabii ambaye walimkufuru, basi ipo nyingine mfano wake au kubwa zaidi kuiliko hiyo kuhusiana na yule waliyemuamini. Basi haikubaki baada ya hayo, isipokuwa matamanio, upendo, na madai matupu ambayo kila mtu anaweza kuyakanusha na mfano wake. Na alipotaja kuwa hawa ndio makafiri wa hakika, akawataja adhabu inayowajumuisha wao na kila kafiri. Akasema, "Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudunisha;" kama walivyofanya kiburi katika kumwamini Mwenyezi Mungu, akawadunisha kwa adhabu chungu yenye hizaya. "Na wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake." Na haya yanajumuisha kuamini kila alilolieleza Mwenyezi Mungu juu ya nafsi Yake, na kila waliloleta Mitume miongoni mwa habari na hukumu mbalimbali. Na hawakutofautisha baina ya yeyote katika Mitume wake, bali waliwaamini wote. Basi hii ndiyo imani ya hakika na yakini iliyojengeka juu ya ushahidi. "Hao atawapa ujira wao;" yaani malipo ya imani yao, yale yaliyotokana nayo ya matendo mema, na maneno mazuri, na tabia nzuri. Kila mmoja kulingana na hali yake. Na pengine hii ndiyo siri katika kufungamanisha malipo nao wenyewe. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Anafuta mabaya, na anakubali mema.