An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُونُوا۟ قَوَّٰمِينَ بِٱلْقِسْطِ شُهَدَآءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمْ أَوِ ٱلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَٱللَّهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا۟ ٱلْهَوَىٰٓ أَن تَعْدِلُوا۟ ۚ وَإِن تَلْوُۥٓا۟ أَوْ تُعْرِضُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ۱۳۵
{135} Yeye Mtukufu anawaamuru waja wake Waumini, “Wawe wenye kusimama imara katika kufanya uadilifu, wenye kushuhudia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Na kusimama imara ni mbinu inayoonyesha wingi wa kitendo hicho. Yani kuweni katika hali zenu zote ni wenye kushikamana na uadilifu, ambao ni kufanya uadilifu katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Bali uadilifu katika haki za Mwenyezi Mungu ni kwamba neema zake zisitumiwe kusaidia kumuasi, bali zitumike katika kumtii Yeye. Na uadilifu katika haki za wanadamu ni kwamba utimize haki zote zinazostahiki kama vile unavyotaka wewe haki zako. Kwa hivyo, unapaswa kutekeleza matumizi ya lazima na madeni, na uamiliane na watu kwa njia ambayo unapenda kwamba waamiliane nawe kwayo miongoni mwa maadili, na malipo, na yasiyokuwa hayo. Na katika kubwa zaidi katika aina za uadilifu ni uadilifu katika kauli na wenye kusema. Basi asiihukumie moja kati ya kauli mbili, au mmoja wa wawili wanaogombana, kwa sababu ya kuhusiana naye, au kuwa na mwelekeo wa upande wa mmoja wao. Bali aufanye mwelekeo wake ni kufanya uadilifu baina yao. Na katika kufanya uadilifu ni kufikisha ushahidi ambao uko nao kwa hali yoyote ulivyo, hata dhidi ya vipenzi, bali hata dhidi ya nafsi yake. Na kwa sababu ya hilo, akasema, "wenye kushuhudia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hata kama ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au fukara, Mwenyezi Mungu ndiye anayewastahiki zaidi." Yaani msimzingatie tajiri kwa utajiri wake, wala masikini kama mnavyodai, kwa kumhurumia. Bali ishuhudieni haki juu ya yeyote yule. Na kutekeleza uadilifu ni miongoni mwa mambo makubwa zaidi na yenye kuonyesha vyema dini ya mwenye kufanya hivyo, na uchamungu wake, na nafasi yake katika Uislamu. Kwa hivyo mwenye kuinasihi nafsi yake, na anataka kuiokoa ni inamlazimu azingatie hilo kuzingatia kukubwa, na kwamba aiweke mbele ya macho yake, na mahali pa lengo lake. Na kwamba aiondolee nafsi yake kila kikwazo na kizuizi kinachomzuia kutaka uadilifu au kuufanyia kazi. Na kizuizi kikubwa zaidi katika hili ni kufuata matamanio. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akatanabahisha juu ya kuondosha kizuizi hiki kwa kauli yake, "Wala msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu." Yaani, msifuate matamanio ya nafsi zenu ambazo zinapingana na haki. kwani, mkiyafuata, mtakengeuka kutoka katika usahihi, na hamtawezeshwa kufanya uadilifu. kwa sababu, matamanio, ima hupofusha ufahamu wa mwenyewe mpaka aione haki kuwa ni batili, na batili kuwa ni haki. Na ima aitambue haki, na aiache kwa ajili ya matamanio yake. Basi mwenye kusalimika na matamanio ya nafsi yake, atawezeshwa kufanya haki na ataongolewa kwenye njia iliyonyooka. Na pale alipobainisha kuwa wajibu ni kufanya uadilifu, akakataza yale yanayopingana na hilo, ambalo ni kupindisha ulimi kutoka katika haki katika ushahidi na mengineyo, na kupotosha matamshi kutoka katika usahihi unaokusudiwa katika kila namna au baadhi ya namna. Na inaingia katika hilo, kupotosha ushahidi na kutoukamilisha au shahidi kuufasiri kwa namna nyingine tu. Basi hakika, hili ni katika kupindisha. Kwa sababu ni kupotoka kutoka katika haki "au mkaupa mgongo." Yaani, kuiacha haki mliyokabidhiwa, kama vile shahidi kuacha ushahidi wake, na hakimu kuacha kuhukumu ambayo ni lazima watekeleze. "Basi hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda." Yaani, ameyazunguka mliyoyafanya, na anayajua matendo yenu, yaliyofichika yake na ya dhahiri yake. Na katika hilo, kuna tishio kali kwa mwenye kupotosha au kupeana mgongo. Na katika mlango wa anayesatahiki zaidi na anayefaa zaidi ambaye anahukumu kwa batili au anashuhudia uwongo. Kwa sababu ni uhalifu mkubwa zaidi. Kwa sababu wale wawili wa kwanza waliiacha haki, naye huyu aliiacha haki na akafanya batili.