پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورهٔ ۴

An-Nisaa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۲۲

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلًا ۱۲۲

Na alipobainisha maishio ya waovu, marafiki wa Shetani, akataja maishio ya wale wenye furaha, marafiki wake, akasema:

{122} Yani "walioamini" Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na majaliwa yake, ya heri yake na ya shari yake, kwa jinsi walivyoamrishwa kwa elimu na kusadiki, na kukiri. "Na wakatenda mema" yanayotokana na imani. Na hilo linajumuisha mambo mengine yote yaliyoamrishwa ya wajibu na yanayopendekezwa, ambayo ni kwa moyo, na kwa ulimi, na kwa viungu vinginevyo vyote. Kila moja lina katika malipo ambayo yaliyofungamanishwa na hayo kulingana na hali yake, na cheo chake, na utimilifu wake wa imani na matendo mema. Na anakosa yale yaliyofungamanishwa na hayo kulingana na yale aliyoshindwa kuyafanya katika imani na matendo. Na hayo ni kulingana na alichojua katika hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema yake. Na vile vile ahadi yake ya kweli ambayo inajulikana kutokana na kufuatilia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake. Na ndiyo maana akataja malipo yanayofungamana na hayo kwa kauli yake, "tutawaingiza katika Bustani zipitazo mito kwa chini yake." Humo kuna ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Miongoni mwa aina za vyakula na vinywaji vitamu, na mambo ya kutazama ya kustaajabisha, na wanandoa wazuri, na majumba na vyumba vilivyopambwa, na miti inayoning'inia, na matunda yasiyo ya kawaida, na sauti nzuri, na neema tele. Na kuwatembelea ndugu na kukumbuka yale waliyokuwa nayo, katika Bustani za Peponi, na juu zaidi kuliko hayo [yote] na matukufu zaidi ni radhi ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na kufurahia kwa roho kwa kuwa karibu na Yeye, na macho kwa kumuona, na masikio kwa maneno yake yatakayowasahaulisha neema zote na furaha. Na kama si tu kuimarishwa kwao na Mwenyezi Mungu, basi wangepepea na kufa kwa sababu ya furaha kubwa. Basi Wallahi, neema gani hii tamu! Na ni ya juu zaidi gani haya aliyowapa Mola Mlezi Mkarimu! Na yale waliyopata ya kila heri na furaha visivyoweza kuelezwa na waelezeaji! Na yenye kutimiza hayo na kuyakamilisha ni kudumu kwa milele katika pahali hapo pa juu zaidi. Ndiyo maana Akasema "Watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli. Na ni nani mkweli zaidi wa kauli kuliko Mwenyezi Mungu?}: Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli, ambaye maneno yake na mazungumzo yake yamefikia kiwango cha juu kabisa kinachowezekana cha ukweli. Na ndiyo maana wakati maneno yake yalipokuwa ni ya kweli, na habari zake ni za kweli; yakawa yale yanayoashiria ni yenye kukubaliana, yenye kujumuisha, na kulazimu. Yote hayo yanakusudiwa katika maneno yake, na vile vile maneno ya Mtume wake – rehema na amani ziwe juu yake. - Kwa sababu yeye hasemi isipokuwa kwa amri yake, na wala hatamki isipokuwa kutokana na wahyi wake.