An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمَن يُشَاقِقِ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ ٱلْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ ٱلْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِۦ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِۦ جَهَنَّمَ ۖ وَسَآءَتْ مَصِيرًا ۱۱۵
{115} Yani, na mwenye kumhalifu Mtume - Rehema na Amani zimshukie - na akampinga katika aliyoyaleta, "baada ya kubainikiwa na uwongofu" kwa hoja za Kiqur-ani na hoja za kinabii. “Na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini.” Na njia yao ni njia yao katika itikadi zao na vitendo vyao. “Tutamuelekeza alikoelekea, “yani tutamwacha na kile alichojichagulia na hatutamsaidia. Kwa hivyo Hatumuwezesha kufikia kheri; Kwa sababu aliiona haki, na akaijua, na akaiacha. Basi Malipo yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa uadilifu ni kwamba amwache katika upotofu wake na akiwa amechanganyika na azidi kupotea juu ya upotovu wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "na walipopotoka, Mwenyezi Mungu akazipotosha nyoyo zao." Na akasema Mwenyezi Mungu, "Nasi tutazigeuza nyoyo zao na macho yao, kama walivyokuwa hawakuyaamini mara ya kwanza." Maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja inaashiria kuwa asiyepingana na Mtume, "na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini." Kwamba makusudio yake yalikuwa ni uso wa Mwenyezi Mungu, na kumfuata Mtume Wake, na kushikamana na umma wa Waislamu, kisha akafanya madhambi au akaingiwa na yale ambayo ni miongoni mwa matakwa ya nafsi na kutawaliwa na maumbile. Basi hakika Mwenyezi Mungu hamwachii nafsi yake na Shetani wake, bali anamwokoa kwa upole wake, na anamneemesha kwa hifadhi yake, na anamkinga kutokana na maovu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuhusu Yusuf, amani iwe juu yake, "Hayo hivyo ni kwa ajili tumwepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu waliosafishwa." Yani kwa sababu ya ikhlasi yake, tulimuepushia maovu, na kadhalika kila mwenye ikhlasi. Kama hili linavyoashiriwa na ujumla wa sababu, na kauli yake, "Na tutamuingiza katika Jahannam;" yani, tutamuadhibu humo adhabu kubwa. "Na hayo ni marejeo maovu zaidi" yani, marejeo yake na maishio.