Az-Zumar
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا مَن شَآءَ ٱللَّهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ ۶۸
{68} Mwenyezi Mungu alipowatia hofu juu ya ukuu wake, akawahofisha kwa hali za Siku ya Kiyama, na akawatia moyo na kuwatisha, akisema: "Na litapulizwa baragumu," ambayo ni pembe kubwa sana na hakuna anayejua ukubwa wake isipokuwa Yule aliyeiumba na wale ambao Mwenyezi Mungu aliwajulisha kuihusu miongoni mwa viumbe wake. Kwa hivyo, ataipuliza mmoja wa Malaika aitwaye Israfil, amani iwe juu yake, ambaye ni Malaika wa karibu na Mwenyezi Mungu na ni mmoja wa wale wanaoshikilia 'Arshi ya Mwingi wa rehema. "Wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi." Walipoisikia sauti yake baragumu hiyo, ikawasumbua kwa sababu ya ukali wake na ukubwa wake, na yale wanayojua kwamba hiyo ni utangulizi wake, "isipokuwa aliyemtaka Mwenyezi Mungu" miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaimarisha lilipopulizwa, kwa hivyo akasalia hajazimika, kama vile waliokufa kwa ajili ya kupigania dini au baadhi yao na wengineo. Huku ndiko kupuliza kwa kwanza ambako kutawazimisha viumbe na kuwafadhaisha. "Kisha litapulizwa mara nyingine" ya pili ambayo nayo ni kwa ajili ya kuwafufua viumbe. "Hapo watainuka" watoke makaburini mwao "wawe wanangojea" ili wafanyiwe hesabu. Hapo watakuwa tayari wamesharudishiwa maumbile yao ya kimwili na kiroho, na macho yao yamekodoka yanangojea kuona wanafanyiwa nini na Mwenyezi Mungu?