پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
سورهٔ ۳۹

Az-Zumar

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۲

ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَٱلَّتِى لَمْ تَمُتْ فِى مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ ٱلَّتِى قَضَىٰ عَلَيْهَا ٱلْمَوْتَ وَيُرْسِلُ ٱلْأُخْرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ۴۲

{42} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye anayewaendesha waja wake katika hali zao za kuwa macho na wanapokuwa usingizini, na katika hali zao za uhai na kifo. Akasema: "Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapokufa" kifo kikubwa kabisa, kifo cha mauti. Kujulisha kwake kuwa Yeye ndiye huchukua roho, na kwamba Yeye ndiye hufanya hivyo, hakupingani na uhakika kuwa ameweka Malaika wa mauti na wasaidizi wake kufanya hivyo. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa juu yenu." Pia akasema: "Mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi kupuuza chochote." Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hujifungamanishia vitu kwa kuzingatia kuwa Yeye ndiye Muumbaji na Mwendeshaji mambo, na pia huvifungamanisha na visababu vyake kwa kuzingatia kwamba ni katika ada yake na hekima yake kwamba aliliwekea kila jambo visababu vyake. Na kauli yake: "Na zile zisizokufa" kifo kidogo "wakati wa kulala kwake," yaani, anaikamata nafsi ambayo haikufa katika usingizi wake. Lakini "huzishika zilizohukumiwa kufa" kati ya nafsi hizi zote, ambazo ni nafsi za wale waliokufa au za wale walioandikiwa kufia kwenye usingizi. "Na huzirudisha nyingine mpaka ufike wakati uliowekwa." "Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri" juu ya ukamilifu wa uwezo wake na kuwafufua wafu baada ya kufa kwao. Katika aya hii, kuna ushahidi kwamba roho na nafsi ni mwili ambao unajisimamia kivyake wala hazifanani na mwili, na kwamba zimeumbwa na zinaendeshwa na Mwenyezi Mungu kwa kuzifisha, kuzishikilia, kuziachilia, na kwamba roho za walio hai na wafu zinakutana kaburini kuzungumza, kisha Mwenyezi Mungu anaziachilia roho za waliohai na kuzishikilia roho za wafu.