Az-Zumar
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلًا فِيهِ شُرَكَآءُ مُتَشَـٰكِسُونَ وَرَجُلًا سَلَمًا لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ۲۹
{29} Kisha akapiga mfano wa shirki na tauhidi, akasema: "Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana." Ni wengi, na hawakubaliani katika jambo wala hali yoyote ili aweze kustarehe. Bali wanagombana kwa sababu yake na kila mmoja wao anayo matakwa anayotaka yatekelezwe, naye mwengine anataka kitu tofauti. Basi, je, unadhani itakuwaje hali ya mtu huyu mbele ya washirika hawa wanaogombana? "Na wa mtu mwengine aliyehusika na bwana mmoja tu" ambaye tayari alishajua makusudio ya bwana wake na akapata raha kamili. "Je, wako sawa katika hali zao?" Hawawi sawa. Basi vile vile, mshirikina ana washirika wanaomgombania. Anamuomba huyu, kisha anamuomba huyu. Kwa hivyo, utamuona hajatulia kokote. Naye anayemkusudia Mola wake Mlezi, Mwenyezi Mungu ameshamuokoa kutokana na ushirikina, basi akawa katika raha na utulivu kamili. "Je, wako sawa katika hali zao? Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu" kwa kubainisha haki mbali na batili, na kuwaongoza wasiojua. "Lakini wengi wao hawajui."