پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saaffaat
سورهٔ ۳۷

As-Saaffaat

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۰۶

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَـٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ ۱۰۶

{106} "Hakika haya" tuliyomtahini kwayo Ibrahim, amani iwe juu yake, "ndiyo majaribio yaliyo dhahiri," ambayo kwayo ulibainika utakaso wa Ibrahim, ukamilifu wa mapenzi yake kwa Mola wake Mlezi na kwamba ni rafiki wake mwandani. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alipomtunuku Ibrahim mwana huyu Ismail, rehema na amani ziwe juu yake, akampenda sana ilhali Ibrahim alikuwa ndiye rafiki mwandani wa Mwingi wa Rehema, ambayo ndiyo daraja ya juu kabisa ya mapenzi na ambayo ni nafasi isiyokubali ushirika kiasi kwamba sehemu zote za moyo zinapaswa kushikamana na mpendwa tu. Basi pindi sehemu moja katika sehemu za moyo wake ziliposhikamana na mwanawe Ismail,Mwenyezi Mungu Mtukufu akataka kuutakasa upendo wake na kuujaribu urafiki wake wa ndani huu. Kwa hivyo akamuamuru amchinje yule ambaye mapenzi yake kwake yalishindana na mapenzi yake kwa Mola wake Mlezi. Na alipoyatanguliza mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuyapendelea kuliko matamanio yake na akaazimia kumchinja, mashindano hayo ya moyoni mwake yakaondoka, basi kukawa kuchinja huko hakuna faida. Ndiyo maana akasema: "Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri."