Faatir
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ ٱلْمُلْكُ ۚ وَٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ۱۳
{13} Na katika masilahi hayo ni kuingiza kwake Mtukufu mchana katika usiku, na usiku katika mchana. Kila moja ya hivyo inapokuja, hicho kingine kinatoweka, na pia moja yake inazidi na nyingine inapunguka na pia vinatoshana. Kwa hivyo yakapatikana kwa sababu ya hayo, masilahi ya waja katika miili yao, wanyama wao, miti yao na mazao yao. Na vile vile Mwenyezi Mungu alivyolitiisha jua na mwezi. Hili lina masilahi ya mwangaza, nuru, mwendo, utulivu, na kuenea kwa waja katika kutafuta fadhila zake, na yaliyomo ndani yake kama vile kuivisha matunda na kukausha yale yanayokauka na mambo mengine miongoni mwa mahitaji ambayo yakipotea, basi watu watadhurika. Na kauli yake: "Kila kimojawapo kinakwenda kwa muda maalumu" anavyotaka Mwenyezi Mungu kikwende. Na muda utakapokuja na mwisho wa dunia ukakaribia, mwendo wake huu utakatika na mamlaka yake yatavurugika, na mwezi utapatwa, na jua litakunjwa, na nyota zitatawanyika. Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoeleza aliyoyaeleza juu ya viumbe hawa wakubwa na mafunzo yaliyomo ndani yao yanayoashiria ukamilifu wake na ukarimu wake, akasema: "Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi," ambaye aliviumba vitu hivi peke yake na akavitiisha, naye ndiye ni Mola Mlezi anayepasa kuabudiwa ambaye ufalme wote ni wake. "Na hao mnaowaomba badala yake" miongoni mwa vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu na masanamu, havimiliki hata "ugozi wa kokwa ya tende." Yaani, hawamiliki chochote, si kidogo wala kichache, hata ugozi wa kokwa ya tende, ambayo ndiyo kitu kinachodharauliwa zaidi. Na huku ni kukanusha kwa ujumla. Vipi wanaabudiwa ilhali hawamiliki chochote katika ufalme wa mbingu na ardhi?