پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
سورهٔ ۲۹

Al-Ankaboot

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۲

قُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ شَهِيدًا ۖ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱلْبَـٰطِلِ وَكَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ۵۲

{52} "Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Shahidi kati yangu na nyinyi" Na mimi ndiye shahidi. Kwa hivyo ikiwa mimi ni mwongo; atanifikishia kile ambacho mtazingatia kwacho. Na ikiwa ananiunga mkono tu, na kuninusuru, na kunisahisishia mambo, basi na uwatoshe ushahidi huu mkubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na ikiwa ilitokea mioyoni mwenu kwamba ushahidi wake - na ilhali hamkumsikia wala hamkumwona - siyo ushahidi wa kuwatosha, basi Yeye "Anayajua yaliyomo katika mbingu na ardhi." Na miongoni mwa yale anayoyajua ni hali yangu na hali yenu, na maneno yangu ninayowaambia. Basi kama ninadanganyishia hayo, naye anajua hilo na ana uwezo wa kuniadhibu; basi hilo lingekuwa la kutia dosari katika elimu yake, uwezo wake, na hekima yake; kama alivyosema Mwenyezi Mungu. "Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu, bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!" "Na wale wanaoiamini batili na wakamkufuru Mwenyezi Mungu, hao ndio waliohasiri." Kwa kuwa walihasiri kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kwa kuwa walipata kila baatili mbaya badala ya haki iliyo sahihi, na wakapata kila adhabu chungu badala ya neema. Basi wakahasiri nafsi zao na familia zao Siku ya Kiyama.