An-Naml
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ سَيُرِيكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ۹۳
{93} "Na sema, "Alhamdu Lillahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu)," ambaye ana sifa katika dunia hii na Akhera, na kutoka kwa viumbe vyote, hasa watu wasomi na wa cheo cha juu mbele yake miongoni mwa waja wake. Kwa maana kile kilichofanyika, na kile kinachofaa kufanyika kutoka kwao cha kumsifu Mola wao Mlezi ni kubwa kuliko kile kinachotokea kutoka kwa wengineo; kwa sababu daraja zao zilizoinuka juu na ukamilifu wa ukaribu wao na Yeye na wingi wa heri zake kwao, "Yeye atawaonyesha Ishara zake, na mtazijua," kujua ambako kutawaonyesha haki na batili. Na ni lazima atawaonyesha ishara zake ambazo kwazo wataangaza giza; ili aangamie mwenye kuangamia kwa ushahidi wa wazi na aishi wa kuishi kwa ushahidi wa wazi. "Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na hayo myatendayo," bali alikwisha yajua matendo mnayoyatenda na hali zenu, na alijua kiasi cha malipo ya matendo hayo, na atahukumu baina yenu kwa hukumu mtakayomsifu juu yake, na wala hamtakuwa na hoja yoyote kwa namna yoyote ile.
Imekamilika tafsiri ya Surat An-Naml kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na wepesishaji wake, na tunamuomba Yeye Mtukufu kwamba zisiache fadhila zake na msaada wake kuendelea kuwa juu yetu na uendelee kutujia kutoka kwake, kwani yeye ndiye mkarimu zaidi wa wakarimu wote, na mbora zaidi wa wanaorehemu, na mwenye kuwaunga waliokatikiwa, na mwenye kuwajibu wanaouliza, na mwenye kurahisisha mambo magumu, na mwenye kufungua milango ya baraka zake, na mwenye kutoa tunu kwa wingi katika wakati wote, na mwenye kurahisisha Qur-ani kwa wanaokumbuka, na mwenye kurahisisha njia zake na milango yake kwa wale wanaomuendea, na anaikunjua meza ya heri zake, na wema wake kuwa wanaotafakari. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad, familia yake na Maswahaba wake. Kimetungwa na mwandishi wake Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah As-Saadi, Mwenyezi Mungu amsamehe, yeye. Na wazazi wake na Waislamu wote. Mnamo Ramadhani 22, 1343. Na kilihaririwa kutoka kwa maandishi ya mwandishi wake tarehe 29 Dhul-Hijjah mnamo 1346.
Imekamilika Sehemu ya tano ya "Taysir Al-Karim Ar-Rahman fi Tafsir Kalam Al-Mannan", na inafuatiwa na sehemu ya sita, ambayo ya kwanza yake ni Tafsiri Surat Al-Qasas. Na inafuatiwa nyuma katika chapisho, kanuni miongoni mwa kanuni za tafasiri, na kutafsiri maneno ya jumla, ambayo yamerudiwa kwa wingi katika Qur-ani, na watu wanahitaji kuyajua.