An-Naml
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ عِلْمًا ۖ وَقَالَا ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّنْ عِبَادِهِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۱۵
{15} Mwenyezi Mungu anataja Katika Qur 'an hii, na kuashiria neema yake juu ya Daudi na Suleiman, mwanawe, kwa kuwapa elimu pana na nyingi. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema katika kauli yake: "Na Daud na Suleiman walipokata hukumu katika kadhiya ya konde walipolisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo. Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu..." mpaka mwisho wa aya. Nao wakasema, wakimshukuru Mola wao Mlezi kwa neema zake kubwa kwa kuwafundisha: "Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa kwote ni kwa Mwenyezi Mungu) aliyetufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini." Kwa hivyo, wakamsifu Mwenyezi Mungu kuwa kuwafanya waumini, watu wa furaha, na kwamba walikuwa wateule miongoni mwao. Na hakuna shaka kwamba waumini wako katika daraja nne: wema, kisha juu yao kuna wale waliokufa kwa ajili ya dini, kisha juu yao kuna wakweli mno, kisha juu yao kuna Manabii. Nao Daudi na Suleiman ni miongoni mwa wateule katika Mitume, hata ingawa wako chini ya daraja la wale Mitume watano wenye azimio kubwa, lakini wao ni miongoni mwa Mitume watukufu, ambao Mwenyezi Mungu aliwataja na kuwasifu katika kitabu chake kwa sifa kubwa. Kwa hivyo, wakamsifu Mwenyezi Mungu kwa kufikia cheo hiki. Na hili ndilo anuani ya furaha ya mja: kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake za kidini na za kidunia, na kuona kwamba neema zote ni kutoka kwa Mola wake Mlezi. kwa hivyo, hajivuni nazo na hazifurahii. Bali anaona kwamba anastahili kushukuru sana juu yake.