Ash-Shu'araa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ رَبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ۲۸
{28} Musa - amani iwe juu yake - akijibu kukanusha kwa Firauni na kumkataa kwake Mola Mlezi wa walimwengu wote, "Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake" miongoni mwa viumbe vingine vyote; "ikiwa nyinyi mnatia akilini." Basi hakika nimekwisha wafikishia ubainisho na kuweka mambo yote wazi kwa namna anayoweza kufahamu yeyote yule aliye na akili hata kidogo tu. Basi mna nini mnapuuza kile ninachowaongelesha nacho? Na katika haya kuna ishara na tanabahisho kwamba yale mliyomtupia Musa kwamba ni wazimu ndio ugonjwa wenu haswa. Kwa maana, kumtupia kwenu kiumbe safi zaidi kiakili na mkamilifu zaidi wao kwa elimu [kwamba ni wazimu], na hali ni kwamba nyinyi ndio vichaa, ambapo akili zenu zilikataa aliye dhahiri zaidi katika kuwepo, Muumba wa dunia na mbingu na vilivyomo kati yake. Kwa hivyo, ikiwa mnamkataa, basi mtathibitisha nini? Na kama mnajifanya kutomjua, basi mnajua nini? Na msipomuamini Yeye na ishara zake, basi mtaamini nini baada ya Mwenyezi Mungu na ishara zake? Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwamba hakika vichaa ambao ni sawa na wanyama wana akili zaidi kuwaliko hawa, na kwamba wanyama wa nyumbani walioachiliwa kula kwa uhuru wao wameongoka zaidi yao.