Al-Furqaan
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَعِبَادُ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى ٱلْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلْجَـٰهِلُونَ قَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۶۳
Kisha akataja miongoni mwa wingi wa heri yake, neema zake kwa waja wake wema, na kuwawezesha kwake kutenda matendo mema yaliyowafanya kupata daraja za juu katika vyumba vya Peponi. Akasema:
{63} Uja kwa Mwenyezi Mungu ni wa aina mbili: uja kwa sababu ya umola wake. Hii wanaingia humo viumbe wote; Waislamu wao na makafiri wao, wema wao na waovu wao. Wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, wanaolelewa na kuendeshwa. "Hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni mja wake." Na uja kwa sababu ya uungu wake, nako ni kumuabudu na rehema zake. Nao ni uja wa manabii wake na vipenzi vyake, ambayo ndiyo umekusudiwa hapa. Na ndiyo sababu akaufungamanisha na jina lake Mwingi wa rehema, ili kuashiria kwamba walifikia hali hii kwa sababu ya rehema yake tu. Kwa hivyo, akataja [kwamba] maelezo yao ndiyo maelezo kamili zaidi, na sifa zao ndizo sifa bora zaidi. Aliwaelezea kwamba ni wale "wanaotembea ulimwenguni kwa staha." Yaani, ni watulivu na wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na viumbe wake. Na hii ni sifa kwao kwamba ni wenye heshima, utulivu na kujiweka chini mbele ya Mwenyezi Mungu na waja wake. "Na wajinga wakiwasemeza" maneno ya ujinga; "hujibu: Salama!" Yaani, wanawaongelesha kwa maneno ambayo wanasalimika kutokana na dhambi, na wanasalimika kutokana na kukabiliana na mjinga kwa ujinga wake. Na huku ni kuwasifu kwa ustahamilivu mkubwa na kumkabili mtenda mabaya kwa wema, kumsamehe mjinga, na akili iliyo sawa ambayo iliwafikisha katika hali hii.