Al-Furqaan
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
تَبَارَكَ ٱلَّذِى جَعَلَ فِى ٱلسَّمَآءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَٰجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا ۶۱
Yeye Mtukufu alirudia katika sura hii tukufu kauli yake, "Ni Mwenye baraka nyingi" mara tatu, kwa sababu maana yake, kama ilivyoelezwa hapo awali, inaonyesha ukuu wake Yeye Muumba, na wingi wa sifa zake, na wingi wa heri zake na hisani zake. Na katika sura hii kuna ushahidi juu ya ukuu wake, upana wa mamlaka yake, kutekelezeka kwa mapenzi yake, ujumla wa elimu yake na uwezo wake, na kuzunguka ufalme wake hukumu za kiamiri na hukumu za kimalipo, na ukamilifu wa hekima yake. Na ndani yake kuna yenye kuonyesha upana wa rehema zake, upaji wake kwa wingi, na wingi wa heri zake za kidini na za kidunia, mambo ambayo yanahitaji kurudiarudia sifa hii nzuri.
{61} Alisema, "Ni Mwenye baraka nyingi yule aliyezijalia nyota mbinguni." Nazo ni nyota kwa ujumla au sehemu ambazo jua na mwezi vinashukia kila sehemu kivyake. Na sehemu hizo ni kama mnara na ngome katika kuuhifadhi mji, na vile vile nyota ni kama minara iliyowekwa kwa ajili ya ulinzi. Kwa maana nyota hizo ndizo wanapigwa kwazo mashetani. "Na akajaalia humo taa" yenye nuru na joto, nayo ni jua, "na mwezi unaong'ara" wenye nuru badala ya joto. Na hili miongoni mwa ushahidi wa ukuu wake na wingi wa ukarimu wake. Kwa maana kile kilicho ndani yake cha uumbaji mzuri zaidi, uendeshaji wenye nidhamu nzuri, na uzuri mkubwa ni ushahidi juu ya ukuu wa muumba wake katika sifa zake zote, na tena yale masilahi na manufaa yaliyo ndani yake kwa viumbe ni ushahidi juu ya wingi wa heri zake.