پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
سورهٔ ۲۵

Al-Furqaan

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۳۳

وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَـٰكَ بِٱلْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا ۳۳

{33} Na ndiyo maana akasema, "Wala hawatakuletea mfano wowote" wanaopinga haki kwa huo na kumkusukuma Mtume kwa huo "isipokuwa na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora zaidi." Yaani, tunakuteremshia Qur-ani inayokusanya haki katika maana zake, na uwazi na ubainisho kamili katika maneno yake. Kwa hivyo maana zake zote ni haki na ukweli ambao hauchafuliwi na batili yoyote wala itikadi potofu kwa njia yoyote ile. Na maneno yake na mipaka yake ya vitu viko wazi zaidi na vimefasiriwa vizuri zaidi, vikibainisha maana kwa njia kamili. Na katika aya hii, kuna ushahidi kwamba mwenye kuzungumza katika elimu, kama vile msimulizi wa hadithi za Mtume, mwalimu, na mtoa waadhi anapaswa kufuata mfano wa Mola wake Mlezi alivyouendesha hali ya Mtume wake. Basi vile vile mwanazuoni anapaswa kuendesha hivyo mambo ya viumbe. Na kila wakati tukio lenye kusababisha jambo au kila msimu fulani unapofika, anatumia aya za Qur-ani na hadithi za Mtume na mawaidha zinazoafikiana na hayo. Na ndani yake kuna jawabu la kuwapinga wale wanaojisumbua kama vile Al-Jahmiyya wanaoona kwamba maandiko mengi ya Qur-ani yanapasa kufahamika kulingana na maana zake za juu juu na kwamba yana maana tofauti na ile inayoeleweka ya kawaida. Kwa hivyo, kulingana na kauli yao hii, Qur-ani haiwi ndiyo tafsiri bora zaidi kuliko vitabu vinginevyo, na kwamba tafsiri iliyo bora zaidi kulingana na madai ati ni tafsiri yao hiyo ambayo walipotosha mno maana yake!