Al-Muminoon
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱدْفَعْ بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ٱلسَّيِّئَةَ ۚ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ ۹۶
{96} Hii ni moja ya maadili matukufu ambayo Mwenyezi Mungu alimwamuru Mtume wake kutekeleza. Akasema: "Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi." Yaani, ikiwa maadui zako wanakuudhi kwa maneno na vitendo, usiwakabili kwa uovu, pamoja na kwamba inafaa kumuadhibu muovu kwa mfano wa maovu yake, lakini kinga maovu yao kwako kwa wema kutoka kwako juu yao. Hii ni fadhila kutoka kwako kwa muovu, na uzuri wa kufanya hivo ni kwamba muovu atapunguza maovu yake kwako kwa muda huu na muda ujao, na kwamba unaita katika kumleta muovu kwenye haki,na humkurubisha zaidi katika kujutia,na kuhuzunika na kutaka toba kwa aliyofanya, na anasifika msamehevu kwa sifa ya ihsani, na kwa hilo humshinda adui yake shetani, na anastahiki thawabu kutoka kwa Mola Mlezi. Amesema Mtukufu: "Lakini mwenye kusamehe,na akasuluhisha, basi malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu." Na Akasema Mtukufu: "Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu." "Lakini hawapewi wema huu." Yaani, haafikiwa kwa tabia nzuri, "ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati. Na kauli yake: "Sisi tunajua wayasemayo;" yaani, wanayoyasema kutokana na maneno yanayojumuisha ukafiri na kukanusha ukweli, hakika imeizunguka elimu yetu kwa hayo, na tumewastahimili, na tumewapa muda na tumekuwa wenye subira kwao, na ukweli ni wetu, na kukanusha kwao kwetu. Ewe, Muhammad, inapaswa uwe na subira kwa yale wanayoyasema, na uwakabili kwa Ihsani. Huu ndio wadhifa wa mja katika kukabili maovu kutoka kwa wanadamu.