Al-Hajj
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لِّيَجْعَلَ مَا يُلْقِى ٱلشَّيْطَـٰنُ فِتْنَةً لِّلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ لَفِى شِقَاقٍۭ بَعِيدٍ ۵۳
{53} Kwa sababu ya utimilifu wa hekima yake, aliwawezesha mashetani kuwafukuza waliotajwa; Ili yatokee yale aliyoyataja katika kusema kwake, "Hayo ni ili alifanye lile analolitia Shetani liwe ni fitna" kwa makundi mawili ya watu ambao Mwenyezi Mungu hajali kuwahusu. [Na hao ndio] "walio na maradhi katika nyoyo zao." Yaani, udhaifu na ukosefu wa imani kamili na imani madhubuti, kwa hiyo shaka ndogo inayojitokeza katika nyoyo zao inawaathiri. Ikiwa walisikia kile Shetani alisema; uoga na shaka vikawaingia, na ikawa ni mtihani kwao. "Na nyoyo zao ni ngumu." Yaani, yule mkali ambaye haathiriwi na karipio wala mawaidha, na haelewi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kutokana na ukali wake. Ikiwa walisikia kile Shetani alisema; wakaifanya kuwa ni udhuru kwa uongo wao, na wakajadiliana nayo, na wakampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ndiyo maana akasema: "Na hakika madhalimu wamo katika kuhitalifiana;" yaani, upinzani kwa Mwenyezi Mungu, upinzani kwa ukweli, na upinzani dhidi yake ni mbali na ukweli. Kile ambacho Shetani atatoa ni majaribu kwa makundi haya mawili, na kitafichua uovu uliofichwa ndani ya mioyo yao.