Al-Anbiyaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِۦ مُشْفِقُونَ ۲۸
{28} Na pamoja na hili, Mwenyezi Mungu alikwisha wazunguka kwa elimu yake, kwa hivyo anajua "yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao" yaani, mambo yao ya zamani na yajayo, na hawatoki kamwe nje ya elimu yake, kama vile hawawezi kutoka nje ya amri yake na uendeshaji wake. Na katika sifa yao ya kutomtangulia kwa neno ni kwamba hawamfanyii uombezi yeyote bila idhini yake na ridhaa yake. Na akiwaruhusu na kumridhia anayefanyiwa uombezi, wanamfanyia uombezi, lakini Yeye Mtukufu haridhii kauli wala kitedo isipokuwa kile ambcho umekusudiwa kwacho uso wake tu, kilichofanywa kwa kumfuata Mtume. Na aya hii ni miongoni mwa ushahidi wa kuthibitisha uombezi, na kwamba malaika watafanya uombezi. "Nao kwa sababu ya kumhofu wanaogopa," na wananyenyekea kwa sababu ya utukufu wake, na nyuso zao zimedhalilika kwa sababu ya utukufu wake na uzuri wake.