Taa-Haa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّى فِى كِتَـٰبٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّى وَلَا يَنسَى ۵۲
{52} Musa akasema, "Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau." Yaani, alikwishayadhibiti matendo yao ya heri na maovu, na akayaandika katika kitabu chake, ambacho ni Ubao uliohifadhiwa, na akayazunguka kwa elimu na kuwa na habari zake zote. Kwa hivyo, hapotei kuhusiana na kitu chochote katika hayo wala hasahau yale anayoyajua katika hayo. Na maana yake ni kwamba waliyaendea yale waliyoyafanya na wakayapata matendo yao, na watalipwa juu yake. Basi hakuna faida yoyote katika kuuliza kwako ewe Firauni juu yao. Kwani huo ni umma uliokwisha pita, watapata yale waliyochuma, nanyi mtapata yale mliyoyachuma. Na ikiwa ushahidi tuliokujia nao na ishara tulizokuonyesha uliyahakikisha kwamba ni ya ukweli na ya yakini, na hiyo ndiyo hali yake ya halisi, basi ifuate haki, na uache kufuru, dhuluma na kujadili katika batili kwa wingi. Na ikiwa una shaka nayo, au uliyaona kwamba si yenye unyoofu, basi njia iko wazi, na mlango wa kufanya utafiti haujafungwa. Basi upinge ushahidi kwa ushahidi, na hoja kwa hoja, lakini hutapata njia yoyote ya kufikia hilo maadamu usiku na mchana bado upo (vinapishana). Vipi aweze hilo, na Mwenyezi Mungu tayari alikwisha julisha kumhusu kwamba alizikanusha ishara ingawa alikuwa na yakini nazo? Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na walizikataa kwa dhuluma na kujivuna, na hali ni kuwa nafsi zao zina yakini nazo." Naye Musa alisema, "Wewe unajua bila ya shaka kwamba hakuna aliyeyateremsha haya isipokuwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili yawe ni ushahidi wa kuonekana." Kwa hivyo ikajulikana kwamba alikuwa dhalimu kakita kujadili kwake, ambaye makusudio yake yalikuwa kujiinua katika ardhi.