پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Taa-Haa
سورهٔ ۲۰

Taa-Haa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۰

قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِىٓ أَعْطَىٰ كُلَّ شَىْءٍ خَلْقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ ۵۰

{50} Musa akajibu kwa jibu la kuridhisha, la kutosha na lililo wazi. Akasema: "Mola wetu Mlezi ndiye aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoza." Yaani, Mola wetu Mlezi ndiye aliyeumba viumbe vyote, na akakipa kila kiumbe umbo lake inavyostahiki, [kuashiria] kazi nzuri ya uumbaji wake, kutokamana na ukubwa wa mwili, udogo wake, wastani wake, na sifa zake zote. Kisha akakiongoza kila kiumbe kwa kile alichokiumbia, na uwongofu huu kamili unaonekana kwa viumbe vyote. Kila kiumbe unachokipata kinatafuta manufaa ambayo kiliumbwa kwa ajili yake katika kuondosha madhara kutoka kwake, Mwenyezi Mungu hata akampa mnyama akili ambayo kwayo ataweza kufanya hivyo, na hii ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu: ''Ambaye amekifanya vizuri kila kitu umbile lake.'' Basi ndiye aliyeumba viumbe, na akawajaalia uumbaji wao mzuri, ambao zaidi ya wema wao akili hazipendekezi, na zikawaongoza kwa maslahi yao. Yeye ndiye Mola Mlezi wa haki; Kukanusha ni kukanusha mambo makubwa zaidi yaliyoko, nayo ni kiburi na kutangaza uongo. Basi lau ingechukuliwa kuwa mtu alikanusha baadhi ya mambo yanayojulikana, hatakataa. Kukanusha kwake Mola Mlezi wa walimwengu kulikuwa kukubwa kuliko hivyo.