Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذْ قُلْتُمْ يَـٰمُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَٰحِدٍ فَٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلْأَرْضُ مِنۢ بَقْلِهَا وَقِثَّآئِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ ٱلَّذِى هُوَ أَدْنَىٰ بِٱلَّذِى هُوَ خَيْرٌ ۚ ٱهْبِطُوا۟ مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ ٱلذِّلَّةُ وَٱلْمَسْكَنَةُ وَبَآءُو بِغَضَبٍ مِّنَ ٱللَّهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَيَقْتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا۟ وَّكَانُوا۟ يَعْتَدُونَ ۶۱
(61) Yani kumbukeni "mliposema" kumwambia Musa kwa namna ya kuchoshwa na kudharau neema za Mwenyezi Mungu. "Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu" yani aina moja ya chakula, ingawa kama ilivyotangulia, kulikuwa na aina mbalimbali, lakini havikuwa vinabadilika. "Basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyomea katika ardhi, kama mboga zake." Yani mimea yake isiyokuwa miti inayosimama juu ya shina lake, "na matango yake, na thom zake, na adesi zake," ambavyo ni vyakula maarufu. Musa akawaambia "Mnabadili kilicho duni" ambavyo ni hivyo vyakula vilivyotajwa, "kwa kile kilicho bora?" Nazo ni Manna na Salwa. Hili haliwafailii. Kwa sababu, vyakula hivi mlivyoviomba, mji wowote mnaotua, humo mtavipata. Na ama chakula chenu ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa hicho ndicho chakula bora na cha heshima. Basi vipi mnaomba badala yake? Na kwa kuwa yale waliyofanya yalikuwa ni dalili kubwa ya subira yao chache, na kudharau kwao maamrisho ya Mwenyezi Mungu na neema zake, akawalipa na malipo kama matendo yao. Akasema: "Na wakapigwa na unyonge" unaoonekana juu ya miili yao "na umasikini" ndani ya nyoyo zao. Kwa hivyo, roho zao hazikuwa za kuheshimika, wala hawakuwa na hima kubwa, bali nafsi zao zilikuwa duni, na azma zao zilikuwa mbaya zaidi "na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu." Yani haikuwa ngawira yao waliorudi nayo na wakafaulu isipokuwa kwamba walirudi na ghadhabu yake juu yao. Basi ngawira mbaya mno ni ngawira yao. Na hali mbaya mno ni hali yao mbaya. "Na hayo" ambayo kwayo walistahiki ghadhabu yake, "ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu," yanayoashiria haki waliyobainishiwa. Basi walipozikataa, akawaadhibu kwa hasira yake juu yao, na kwa yale waliyokuwa "wakiwauwa Manabii pasipo haki." Na kauli yake "pasipo haki." Ni ziada ya kuonyesha ubaya wa hilo. Vinginevyo inajulikana kuwa siyo haki kumuua Nabii, lakini (hili neno liliongezwa) ili usije ukafikiriwa ujinga wao na kutojua kwao. "Hayo ni kwa walivyoasi" kwa kuwa walimuasi Mwenyezi Mungu "na wakapindukia mipaka." dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu maasia yanaitana yenyewe kwa yenyewe. Na kughafilika kunasababisha dhambi ndogo, kisha yanatokana na hilo madhambi makubwa, kisha zinatokana na hilo aina mbali mbali za uzushi, ukafiri na mengineyo. Hivyo basi, tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde kutokana na kila balaa. Na jua ya kwamba maneno katika Aya hizi yamekusudiwa umma wa Wana wa Israili waliokuwepo wakati wa kuteremka kwa Qur-ani. Na hivi vitendo vilivyotajwa waliongeleshwa wao kwavyo, ingawa ni vitendo vya mababu zao. Na walinasibishwa navyo kwa faida mbalimbali. Miongoni mwake ni kwamba walikuwa wakijisifu na wakizitakasa nafsi zao, na wanadai kuwa wao ni bora kumliko Muhammad na wale waliomwamini. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akabainisha katika hali za watangulizi (mababu) zao ambazo walikwisha jua vizuri kile kinachomwekea wazi kila mmoja wao kwamba wao si miongoni mwa watu wenye subira, na maadili mema, na matendo ya juu. Basi ikiwa hii ndiyo hali ya watangulizi wao - pamoja na kwamba dhana kubwa ni kuwa wao (watangulizi) wanastahili na ni wa hali ya juu zaidi kuliko wale wa baada yao – basi itakuwa vipi dhana juu ya wale wanaoongeleshwa. Na miongoni mwake ni kwamba neema ya Mwenyezi Mungu juu ya waliotangulia miongoni mwao ni neema ya kuendelea hadi kwa waliokuja baadaye. Na neema juu ya mababa ni neema juu ya watoto. Kwa hivyo, wakaongeleshwa kwazo (hizo neema), kwa sababu ni neema zinazowaenea na kuwajumuisha. Na miongoni mwake ni kwamba kuwaongelesha kwa vitendo vya wengine, ni katika yale yanayoashiria kuwa umma uliokusanyika juu ya dini moja, unategemeana na kusaidiana kwa masilahi yake, kiasi kwamba ni kama kwamba wa kwanza na wa mwisho wao wako katika wakati mmoja. Na ni kama kwamba tukio la baadhi yao ni tukio kutoka kwa wote. Kwa sababu anachoyafanya mmoja wao katika kwa heri, inaleta masilahi ya wote. Na anachoyafanya katika maovu, madhara yake yanawarudia wote. Na miongoni mwake ni kwamba wao hawakupinga mengi ya matendo yao (yani ya mababu zao). Na mwenye kuridhia uasi, basi yeye ni mshiriki wa huyo muasi, na mengineyo miongoni mwa hekima ambazo hazijui isipokuwa Mwenyezi Mungu.