Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَٱكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌۢ بِٱلْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ ٱللَّهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ ٱلَّذِى عَلَيْهِ ٱلْحَقُّ وَلْيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْـًٔا ۚ فَإِن كَانَ ٱلَّذِى عَلَيْهِ ٱلْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُۥ بِٱلْعَدْلِ ۚ وَٱسْتَشْهِدُوا۟ شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَٱمْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ ٱلشُّهَدَآءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَىٰهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَىٰهُمَا ٱلْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ ٱلشُّهَدَآءُ إِذَا مَا دُعُوا۟ ۚ وَلَا تَسْـَٔمُوٓا۟ أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰٓ أَجَلِهِۦ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ ٱللَّهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَـٰدَةِ وَأَدْنَىٰٓ أَلَّا تَرْتَابُوٓا۟ ۖ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَـٰرَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوٓا۟ إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَآرَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا۟ فَإِنَّهُۥ فُسُوقٌۢ بِكُمْ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱللَّهُ ۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ ۲۸۲
{282} Aya hizi zinajumuisha Al-Bari (Muumba mwanzilishi) kuwaelekeza waja wake katika kuamiliana kwao. Kwamba wahifadhi haki zao kwa njia zenye manufaa na marekebisho ambayo hawawezi watu wenye hekima kupendekeza kilicho juu zaidi wala kamili zaidi kuliko hili. Kwani ndani yake kuna manufaa mengi: Miongoni mwake ni kuruhusika kufanya miamala katika madeni, sawa yawe ni madeni ya Salam, au kununua ambako thamani italipwa baadaye. Yote hayo yanaruhusika, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliyajulisha kuhusu Waumini. Na lolote alilojulisha kuhusu Waumini, hilo ni miongoni mwa matakwa ya imani. Na aliwakubalia hilo yeye Mfalme, Atakayehesabu matendo yao. Na miongoni mwake ni ulazima wa kutaja muda maalumu katika madeni yote, na muda wa mwisho wa mikataba ya kukodisha. Na miongoni mwake ni kwamba, ikiwa muda haujulikani, basi hilo haliruhusiki. Kwa sababu ni udanganyifu na hatari, hivyo linaingia katika kamari. Na miongoni mwake, ni amri yake Mola Mtukufu ya kuyaandika madeni. Na amri hii inaweza kuwa wajibu inapokuwa ni wajibu kuihifadhi haki. Kama ile ambayo ni ya mja aliye katika ulinzi wake, kama vile mali za mayatima, na wakfu, na mawakala na wadhamini. Na inaweza kukaribia kuwa wajibu kama vile inapokuwa haki ni ya mtu mwenyewe peke yake. Basi ulazima unaweza kuwa na nguvu, na (kusamehe na) kutarajia malipo kwa Mwenyezi Mungu kulingana na hali zinazolazimu hilo. Na kwa vyovyote vile, kuandika ni katika mambo makubwa zaidi ambayo miamala hii ya baadaye huhifadhiwa kwayo. Kwa sababu ya wingi wa usahaulifu na kutokea kwa makosa, na kwa ajili ya kuilinda dhidi ya wasaliti ambao hawamchi Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na miongoni mwake, ni amri yake Mola Mtukufu kwamba mwandishi andike baina ya wawili wanaoamiliana kwa uadilifu. Wala asiegemee upande wa mmoja wao kwa sababu ya ujamaa kati yao au kitu kinginecho. Wala dhidi ya mmoja wao sababu ya uadui kati yao na mfano wake. Na miongoni mwake ni kwamba, kuandika baina ya wale wanaoamiliana ni miongoni mwa matendo bora kabisa zaidi, na ni miongoni mwa kuwatendea wema. Na ndani yake kuna kuhifadhi haki zao na kuwafanya kutokuwa na hatia, kama Mwenyezi Mungu alivyomwamrisha kufanya hivyo. Basi mwandishi kati ya watu na atarajie malipo kwa Mwenyezi mungu juu ya mambo haya ili apate thawabu zake. Na miongoni mwake ni kwamba, mwandishi ni lazima atambue uadilifu na ajulikane kwa uadilifu. Kwani asipoujua uadilifu, basi hataufikia. Na akiwa hazingatiwi kuwa mwadilifu kwa watu mwenye kuridhiwa, basi kuandika kwake huko hakutazingatiwa. Na wala makusudio ambayo ni kuhifadhi haki, hayatafikiwa kupitia kuandika huko. Na miongoni mwake ni kwamba, katika ukamilifu wa uandishi na uadilifu katika hilo ni kwamba mwandishi awe na utunzi mzuri. Na utumizi wa maneno yanayozingatiwa katika kila muamala kwa mujibu wake. Na desturi katika suala hili ina mazingatio makubwa. Na miongoni mwake ni kwamba, uandishi ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake; ambao mambo yao ya kidini wala ya kidunia hayanyooki isipokuwa kwayo. Na kwamba yule ambaye Mwenyezi Mungu alimfundisha kuandika, basi amempa fadhila kubwa. Basi katika ukamilifu wa shukrani yake juu ya neema hiyo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuwatimizia waja mahitaji yao kwa kuandika kwake huko, wala asikatae kuandika. Na kwa sababu, akasema, "wala mwandishi asikatae kuandika kama alivyomfunza Mwenyezi Mungu." Na miongoni mwake ni kile anachoandika mwandishi ni kukiri kwa yule ambaye haki iko juu yake ikiwa ana uwezo wa kuieleza haki ambayo iko juu yake. Na ikiwa hawezi kufanya hivyo vizuri kwa sababu ya umri wake mdogo, au upumbavu wake, au wazimu wake, au ububu wake au kutokuwa na uwezo kwake; basi mlinzi wake atamwandikishia, na mlinzi wake atachukua mahali pake. Na miongoni mwake ni kwamba, kukiri ni katika njia kubwa zaidi ambazo haki huthibitishwa. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoamrisha kwamba, mwandishi aandike yale aliyoandikishwa na yule ambaye deni liko juu yake. Na miongoni mwake, ni kuwepo kwa ulinzi juu ya wale wasiojiweza kama vile watoto, wendawazimu, wapumbavu, na mfano wao. Na miongoni mwake ni kwamba, mlinzi anachukua nafasi ya mlezi wake katika kukiri kwake kwote kunakohusiana na haki zake. Na miongoni mwake ni kwamba, yule unayemkabidhi amana katika muamala na ukamkabidhi usimamizi katika hilo; basi kauli yake katika hilo inakubalika, naye ni mwakilishi wako. Kwa sababu ikiwa mlezi wa wasiojiweza anafanya kwa niaba yao, basi yule uliyempa mamlaka kwa uteuzi wako na ukamkabidhi jambo lako anastahiki zaidi kukubaliwa, na kuzingatiwa kauli yake na kuitanguliza mbele ya kauli yako iwapo kuna hitilafu. Na miongoni mwake ni kwamba, ni wajibu juu ya yule ambaye haki iko juu yake anapomwandikisha mwandishi amche Mwenyezi Mungu; na wala asipunguze haki ambayo iko juu yake. Basi na asipunguze katika kiwango chake wala maelezo yake, wala katika sharti miongoni mwa masharti yake wala kikwazo katika vikwazo vyake. Bali ni juu yake akiri kila anachodaiwa na vinavyoambatana na haki hiyo. Na hilo linavyokuwa wajibu ikiwa ni haki yake juu ya wengine. Kwa hivyo asiyefanya hivyo, basi yeye ni miongoni mwa wapunjao, wapunguzao. Na miongoni mwake ni ulazima wa kukiri haki zilizo dhahiri, na haki zilizofichika, na kwamba hilo ni katika kubwa zaidi ya sifa za uchamungu. Kama vile kuacha kuzikiri ni miongoni mwa yale yanayobatilisha uchamungu na yenye kuupunguza. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kushuhudisha katika mauziano. Na ikiwa ni katika kudaiana, basi hukumu yake ni sawa na hukumu ya kuandika kama ilivyotangulia. Kwa sababu, kuandika ni kuandika ushahidi. Na ikiwa mauziano ni ya papo hapo, basi inapaswa kushuhudiwa hilo. Lakini hakuna ubaya kuacha kuandika kwa sababu ya wingi wake na kutokea kwa ugumu ndani yake. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kuwashuhudisha wanaume wawili waadilifu. Na ikiwa hawapo, au haiwezekani, au ni vigumu, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili. Na hilo linajumuisha maamiliano yote. Mauziano ya papo hapo, na mauziano kwa mkopo, na yale yanayoambatana nayo kama vile masharti na hati na mengineyo. Na ikisemekana kwamba imethibiti kwamba yeye, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alihukumu kwa ushahidi wa mtu mmoja pamoja na kiapo. Ilhali Aya hii tukufu haina isipokuwa ushahidi wa wanaume wawili au mwanamume mmoja na wanawake wawili. Itasemwa: Aya hii tukufu ina mwongozo wa Al-Bari (Muumba mwanazilishi) kwa waja wake katika kuzihifadhi haki zao. Na kwa sababu hii ndiyo akaweka ndani yake njia kamili zaidi ya hilo na yenye nguvu zaidi. Na hakuna chochote ndani yake kinachopingana na alichotaja Nabii, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - cha kuhukumu kwa shahidi mmoja na kiapo. Kwa hivyo, mlango wa kuhifadhi haki mwanzo kwa jambo hilo, mja anaelekezwa katika hilo kutahadhari na kuhifadhi kikamilifu. Na mlango wa kuhukumu baina ya wanaogombana hapo inaangaliwa kilicho sahihi zaidi na maelezo kulingana na hali zake. Na miongoni mwake ni kwamba, ushahidi wa wanawake wawili unasimama katika nafasi ya mwanamume mmoja katika haki za kidunia. Ama katika mambo ya kidini, kama vile riwaya (ya Qurani na hadithi) na fatwa, basi mwanamke katika hayo anasimama katika nafasi ya mwanamume mmoja. Na tofauti iko wazi baina ya milango hii miwili. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kwenye hekima katika ukweli kwamba, ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahidi wa mwanamume mmoja. Na kwamba kwa sababu ya udhaifu wa kumbukumbu za mwanamke mara nyingi, na nguvu ya kumbukumbu ya mwanamume. Na miongoni mwake, ni ikiwa shahidi atasahau ushahidi wake, na shahidi mwingine akamkumbusha naye akakumbuka, kwamba hakudhuru kusahau huko kunapoisha. Kwa sababu ya kauli yake, "ili akisahau mmoja wao, basi mmoja wao atamkumbusha huyo mwingine". Na hata la aula zaidi ni kwamba shahidi akisahau, kisha akakumbuka bila ya kukumbushwa, basi ushahidi unazunguka kwenye elimu na yakini. Na miongoni mwake, ni ushahidi ni lazima uwe kutokana na elimu na yakini, na siyo kutokana na shaka. Na pindi shahidi atakuwa na shaka katika ushahidi wake, hata ikiwa ni uwezekano mkubwa tu wa shaka; basi haiwi halali kwake kushuhudia isipokuwa kwa anachokijua. Na miongoni mwake, ni kwamba shahidi hana haki ya kukataa akiitwa kutoa ushahidi, sawa aliitwa kusikiliza au kutoa ushahidi. Na kwamba kutoa ushahidi ni miongoni mwa matendo mema yaliyo bora zaidi. Kama alivyoamrisha kwalo Mwenyezi Mungu na akajulisha kuhusu manufaa yake na masilahi yake. Na miongoni mwake ni kwamba, siyo halali kumdhuru mwandishi au shahidi kwa kuwaita katika wakati au hali inayoweza kuwadhuru. Kama vile lilivyo katazo kwa wenye haki na wale wanaoamiliana kuwadhuru mashahidi na waandishi. Na vile vile ni katazo kwa mwandishi na shahidi kuwadhuru wale wanaoamiliana au mmoja wao. Na katika hili pia, ni kwamba ikiwa shahidi na mwandishi watapatwa na madhara katika kuandika na kushuhudia, basi ulazima unawaondokea. Na miongoni mwake, ni kupeana tanbihi kwamba wahisani wote wanaofanya wema siyo halali kuwadhuru na kuwabebesha wasiyoyaweza. Kwani malipo ya ihsani siyo (kingine) isipokuwa ihsani? Basi vile vile, mwenye kufanya hisani na akatenda wema ni juu yake kukamilisha ihsani yake hiyo, kwa kuacha kuwadhuru kimaneno na kikauli wale aliowafanyia wema; kwa sababu ihsani haikamiliki isipokuwa kwa hilo. Na miongoni mwake ni kuwa, hairuhusiki kuchukua malipo kwa ajili ya kuandika na kutoa ushahidi pale inapolazimu. Kwa sababu ni haki ambayo Mwenyezi Mungu ameilazimisha juu ya mwandishi na shahidi, na kwa sababu ni katika kuwadhuru wale wanaoamiliana. Na miongoni mwake ni tanbihi juu ya masilahi na manufaa yanayotokana na kutenda kulingana na maelekezo haya makubwa. Na kwamba yamo kuhifadhiwa kwa haki, na uadilifu, na kukata migogoro. Na kuwa usalama kutokana na kusahau na kupoteza mawazo. Na ndiyo maana akasema: "Hayo ndiyo uadilifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na ya chini zaidi kuwafanya msiwe na shaka". Haya ni masilahi ya lazima ya waja. Na miongoni mwake ni kwamba kujifunza kuandika ni miongoni mwa mambo ya kidini. Kwa sababu ni njia ya kuhifadhi dini na dunia, na ni sababu ya kufanya wema. Na miongoni mwake ni kwamba, mwenye kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa kumpa neema fulani miongoni mwa neema wanazozihitaji watu, basi katika ukamilifu wa kuzishukuru neema hizi ni kuzirudisha kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Na kuwatimizia mahitaji yao kwazo, kwa sababu Mwenyezi Mungu alifanya sababu ya kumkataza kuandika, kwa kumkumbusha mwandishi juu ya kauli yake. "Kama Mwenyezi Mungu alivyomfundisha." Pamoja na hayo, yeyote anayemkidhia ndugu yake mahitaji, basi Mwenyezi Mungu atamkidhia mahitaji yake. Na miongoni mwake ni kwamba kuwadhuru mashahidi na mwandishi ni kuruka mipaka kwa mtu. Kwa sababu Al-Fusuuq ni kutoka katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kumuasi. Nayo huongezeka na hupungua na inagawanyia sehemu. Na ndiyo maana hakusema, "basi nyinyi ni mafasiki (yani mtu kutoka katika utiifu)." Bali alisema, "basi hakika huko ni kupita mipaka mliko nako." Na kwa kiwango cha mja kutoka katika utiifu wa Mola wake Mlezi, basi anatoka katika mipaka kulingana na hilo. Na kauli ya Mwenyezi Mungu, "na mcheni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawafundisha," ilitumika kama ushahidi kwamba uchamungu ni njia ya kupata elimu. Na iliyo wazi zaidi kuliko hiyo ni kauli yake Mtukufu. "Enyi mlioamini, ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuzi." Yani elimu ambayo kwayo mnatofautisha baina ya uhakika, haki na batili. Na miongoni mwake ni kwamba, kama ilivyo elimu yenye manufaa kujifundisha mambo ya kidini yanayohusiana na ibada. Pia katika hilo ni kujifundisha mambo ya kidunia yanayohusiana na miamala. Kwa maana, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewahifadhia waja mambo ya dini yao na dunia yao, na kitabu chake kitukufu kimo ubainisho wa kila kitu. Na miongoni mwake ni uhalali wa kudhamini haki, ambako ni rehani na dhamana ambazo zinamhakikishia mja kwamba atapata haki yake. Sawa awe anaamiliana na mtu mwema au muovu, mkweli au msaliti. Na ni kwa dhamana ngapi ambazo zinazohifadhiwa haki na kukata migogoro. Na miongoni mwake ni kwamba ukamilifu wa dhamana katika rehani ni kwamba iwe imepokewa tayari. Na hilo halionyeshi kwamba rehani siyo halali isipokuwa kwa kuipokea. Bali kutaja hususan kuwa rahani iwe imepokewa kunaashiria kwamba, inaweza kuwa imepokewa kupokewa kunakoleta dhamana kamili. Na huenda ikawa haijapokewa, kwa hivyo ikawa pungufu. Na miongoni mwake ni kwamba ushahidi unachukuliwa katika kauli yake: