Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُبْطِلُوا۟ صَدَقَـٰتِكُم بِٱلْمَنِّ وَٱلْأَذَىٰ كَٱلَّذِى يُنفِقُ مَالَهُۥ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۖ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُۥ وَابِلٌ فَتَرَكَهُۥ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَىْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ ۲۶۴ وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمُ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍۭ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَـَٔاتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ۲۶۵ أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُۥ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ لَهُۥ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَأَصَابَهُ ٱلْكِبَرُ وَلَهُۥ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَآءُ فَأَصَابَهَآ إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَٱحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ۲۶۶
{264 - 266} Katika Aya hizi, Mwenyezi Mungu alipiga mifano mitatu: Kwa yule anayetoa kwa ajili ya kutafuta uso wake, na hakukifuatisha alichokitoa masimbulizi wala maudhi. Na kwa yule aliyekifuatisha masimbulizi na maudhi, na kwa anayejionyesha (katika kutoa). Ama huyo wa kwanza, pale kutoa kwake kwa ajili ya matumizi kulipokubaliwa, kwenye kuzidishwa maradufu kwa sababu kulitoka kwa imani na ikhlasi kamili. "Kwa kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao." Yani wanatoa na hali wamesimama imara kwa namna ya kufanya ukarimu na ukweli, basi mfano wa matendo haya "ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu." Napo ni mahali palipoinuka juu kwa sababu huwa panaonekana wazi kwa upepo na jua, na maji ndani yake ni mengi. Na hata kama mvua hiyo kubwa isipoinyea, inakuwa na umande wa kutosha kwa sababu ya uzuri wa mimea yake, na uzuri wa ardhi yake, na kupatikana kwa sababu zote zinazoleta kukua kwake, na kustawi kwake na kuzaa kwake. Na kwa sababu hii "ikaleta mazao yake maradufu" yani ikawa imezidishwa mizidisho. Na pepo hii iliyo na sifa hizi ndiyo ya juu zaidi wanayoiomba watu, kwani matendo mema yanalipwa kwa daraja za juu kabisa. Na ama mwenye kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akafuatisha kutoa kwake masimbulizi na maudhi, au alifanya kitendo kisha akafanya cha kukibatilisha kitendo hicho, basi huyu mfano wake ni mfano wa mwenye hii bustani. Lakini ilitumiwa "kimbunga chenye moto, kwa hivyo ikaungua" ilhali ana dhuria dhaifu, naye pia ni dhaifu amekwisha patwa na uzee. Basi hali hii ni miongoni mwa hali za kutisha sana, na ndio maana alianzisha huu mfano kwa kauli yake. "Je, angependa mmoja wenu" hadi mwisho wake kwa swali linalojulikana kwa anayeongeleshwa kutisha kwake. Kwa maana, kuharibika kwake mara moja baada ya miti yake kuchanua na matunda yake kuiva, ni msiba mkubwa. Kisha kupatikana kwa huu mpigo hali ya kuwa mwenyewe ni mzee ambaye ameshadhoofika kufanya kazi. Naye ana dhuria dhaifu ambao hawawezi kumsaidia na hata matumizi yao yako juu yake ni msiba mwingine. Basi akawa mwenye mfano huu, ambaye alifanya matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kisha akayabatilisha matendo yake kwa chenye kuyapinga inafanana na hali ya yule mwenye bustani ambayo yaliifanyikia yale yaliyofanyika wakati alipokuwa anaihitaji sana. Mfano wa tatu ni yule anayejionyesha kwa watu na hana imani kwa Mwenyezi Mungu wala hatarajii malipo yake mazuri. Kwani moyo wake unafananishwa na jiwe linaloteleza lenye udongo juu yake. Mwenye kuangalia atadhani kwamba mvua ikilinyeshea litaotesha mimea kama zinazvyootesha mimea ardhi nzuri. Lakini hili ni kama jiwe lililonyeshewa na mvua kubwa na ikaondoa udongo uliokuwa juu yake na ikaliacha tupu. Na huu ni mfano unaolingana na moyo wa yule anayejionyesha kwa watu ambao hauna imani. Bali yeye ni mgumu na wala halainiki wala hanyenyekei. Basi haya ndiyo matendo yake na kutoa kwake, havina msingi wa kuvisimamisha juu yake wala mwisho ambao vinaishia. Bali alichokifanya ni batili kwa sababu hakikuwa na masharti yake. Na kilicho kabla yake kilibatilika baada ya kupatikana kwa sharti kwa sababu ya kuwepo kizuizi. Na la kwanza lilikubaliwa na linazidishwa maradufu kwa sababu ya kuwepo kwa sharti lake ambalo ni imani na ikhlasi na uimara, na kutokuwepo vizuizi vyenye kuharibu. Na mifano hii tatu inaingia vizuri juu ya watenda matendo wote. Basi mja aipime nafsi yake na wengine kwa mizani hizi ya uadilifu na mifano inayolingana. "Na hiyo mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu isipokuwa wenye elimu."