پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۵۵

ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْحَىُّ ٱلْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُۥ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشْفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذْنِهِۦ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىْءٍ مِّنْ عِلْمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ ۖ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْعَظِيمُ ۲۵۵

{255} Alisema (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba, Aya hii ndiyo kubwa zaidi katika Aya za Qur-ani. Kwa sababu ya kile ilichojumuisha cha maana ya Tauhidi, ukubwa, na wingi wa sifa za Al-Bari (Muumba mwanzilishi) Mtukufu. Alisema kuwa yeye ni "Allah (Mwenyezi Mungu)" ambaye ana maana zote za uungu. Na kwamba hakuna anayestahiki uungu na ibada isipokuwa Yeye tu. Kwani, uungu wa asiyekuwa Yeye na ibada ya asiyekuwa Yeye ni batili, na kwamba yeye ndiye "Al-Hayyu (Aliye hai)." Ambaye ana maana zote za uhai mkamilifu kama vile kusikia, kuona, nguvu, kutaka (mapenzi), na sifa nyinginezo miongoni mwa sifa za kibinafsi. Kama vile "Al-Qayyum (Msimamia mambo yote)" ambayo zinaingia ndani yake Sifa zote za kimatendo. Kwa sababu Yeye ndiye Msimamizi ambaye anajisimamia mwenyewe bila ya kuvihitaji viumbe vyake vyote. Na alivisimamia vyote vinavyopatikana kwani aliviumba vyote, na akavifanya kuendelea kuwepo. Na akavipa kila vinachohitaji kwa ajili ya kuwepo kwake na kuendelea kwake kuishi. Na katika ukamilifu wa uhai wake na Usimamizi wake ni kwamba "hashikwi na kusinzia wala kulala". Kwa sababu, kusinzia na kulala huwa vinampata kiumbe ambaye amepatwa na udhaifu, kutoweza na kuharibika. Na wala havimpati yule mwenye Ukuu, Ukubwa, na Utukufu. Na katika ukamilifu wa ufalme wake ni kwamba "hafanyi uombezi mbele yake" yeyote "isipokuwa kwa idhini yake". Kila wenye heshima, na waombezi wote ni waja wake, na wanamilikiwa na wala hawajitokezi kufanya uombezi mpaka awape idhini. "Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi." Na Mwenyezi Mungu hamruhusu yeyote kufanya uombezi isipokuwa kwa anayemridhia. Na wala haridhii isipokuwa kumpwekesha na kuwafuata Mitume wake. Kwa hivyo, asiyesifika kwa haya, basi hana fungu lolote katika uombezi. Kisha akajulisha kuhusu elimu yake pana inayoenea, na kwamba anayajua yaliyo mbele ya viumbe ya mambo yajayo ambayo hayana mwisho. “Na yaliyo nyuma yao” katika mambo yaliyopita ambayo hayana mpaka, na kwamba haifichiki siri yoyote kwake. “Anajua hiyana ya macho na vinavyoficha vifua.” Na kwamba, yeyote katika viumbe hajui vyema chochote katika elimu ya Mwenyezi Mungu na habari zake. “Isipokuwa kwa kile atakacho” katika hayo. Nayo ni yale aliyowafahamisha katika mambo ya kisheria na ya majaaliwa. Nayo ni sehemu ndogo sana ya elimu yenye kuisha (kwa viumbe) katika elimu za Al-Bari (Muumba mwanzilishi) na habari zake. Na kama walivyosema wenye kumjua zaidi kati ya viumbe, ambao ni Mitume na Malaika; “Subhanaka (Wewe umetakasika)! Hatuna elimu isipokuwa kile ulichotufunza”. Kisha akajulisha kuhusu ukuu wake na utukufu wake, na kwamba Kursi yake imeenea mbingu na ardhi. Na kwamba amehifadhi vyote viwili na vilivyomo miongoni mwa walimwengu kwa njia (sababu) na mifumo ambayo Mwenyezi Mungu aliweka katika viumbe. Hata hivyo, halemewi, yani haimuwii vigumu kuvihifadhi vyote viwili kwa sababu ya ukamilifu wa ukuu wake, uwezo wake, na upana wa hekima yake katika hukumu zake. “Na Yeye ndiye aliye juu zaidi” kwa dhati yake juu ya viumbe vyake. Naye ndiye aliye juu zaidi kwa ukuu wa sifa zake. Naye ndiye aliye juu zaidi ambaye amevishinda nguvu viumbe, na vyote vilivyo chini ya hukumu yake, na magumu yote yamenyenyekea, na shingo zote zimemdhalilikia. “Mkuu” aliyekusanya sifa zote za ukuu, ukubwa, utukufu, uzuri ambaye anapendwa na nyoyo, na roho zinamtukuza. Na wale wanaojua wanajua kwamba ukuu wa kila kitu, hata ukiwa mkuu vipi kwa sababu ya sifa zake, basi huo hupunguka kwa kulinganisha na ukuu wa Al-‘Ali (Mtukufu), Al-‘Adhim (Mkuu). Ni Aya iliyojumuisha maana hizi ambazo ni katika maana tukufu zaidi ina haki ya kuwa kubwa zaidi katika Aya za Qur-ani. Na mwenye kuisoma kwa kutafakari na kuelewa anayo haki ya moyo wake kujaa yakini na shukran na imani, na kwamba ahifadhiwe kwa hayo kutokana na shari ya Shetani.