پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۳۳

وَٱلْوَٰلِدَٰتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَـٰدَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ ٱلرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى ٱلْمَوْلُودِ لَهُۥ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَآرَّ وَٰلِدَةٌۢ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُۥ بِوَلَدِهِۦ ۚ وَعَلَى ٱلْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوٓا۟ أَوْلَـٰدَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّآ ءَاتَيْتُم بِٱلْمَعْرُوفِ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ۲۳۳

{233} Hii ni habari yenye maana ya amri, kwa kuiteremsha katika hali ya kile ambacho kimeshathibiti, kisichohitaji kuamrishwa kwamba, "na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili". Na kwa kuwa mwaka huitwa hivyo ukiwa kamili, au sehemu ya kubwa ya mwaka. Akasema, "kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha." Kwa hivyo, mtoto anayenyonya anapokamilisha miaka miwili, basi kunyonya kwake kutakuwa kumekamilika. Na yanakuwa maziwa hayo baada ya hapo kama vyakula vinginevyo. Kwa hivyo, kunyonyesha baada ya miaka miwili hakuzingatiwi na wala hakuharamishwi. Na inachukuliwa kutoka katika andiko hili na katika kauli yake Mola Mtukufu. "Na mimba yake na kumwachisha kwake kunyonya ni miezi thelathini." Kwamba muda wa chini zaidi wa ujauzito ni miezi sita, na kwamba inawezekana mtoto kuwepo ndani yake. "Na ni juu ya aliyezaliwa mwana," yani baba yake, "chakula chao na kuwavalisha mavazi yao kwa wema". Na hili linajumuisha ikiwa yupo chini yake au ametalikiwa. Basi ni juu ya baba (ya mwana) ruzuku yao, yani kumpa matumizi na mavazi, na kila mmoja ni kulingana na hali yake. Ndiyo maana Mola Mtukufu akasema: "Wala halazimishwi mtu isipokuwa kwa kiwango cha uwezo wake". Hivyo basi, fakiri hatakiwi kutoa matumizi ya tajiri, wala yule ambaye hana chochote kwamba atoe, mpaka apate. "Mama asitaabishwe kwa sababu ya mwanawe, wala yule aliyezaliwa mwana kwa sababu ya mwanawe." Yani sio halali mama kudhuriwa kwa sababu ya mwanawe, ima kwa kumzuia kumnyonyesha au kutompa anachotakiwa cha matumizi, na mavazi, au kodi (ujira). "Wala yule aliyezaliwa mwana kwa sababu ya mwanawe." Kwa mama kukataa kumnyonyesha kwa kutaka kumdhuru [baba] au kumuomba (baba) zaidi ya kile kilicho wajibu, na mfano wa hayo miongoni mwa aina za madhara. Na iliashiria kauli yake, "yule aliyezaliwa mwana" kwamba mtoto ni wa baba yake; kwa sababu alipewa kama zawadi, na kwa sababu ni kutokana na alichochuma. Na ndiyo maana inaruhusika kwake kuchukua katika mali yake, aridhie au asiridhie, tofauti na mama. Na kauli yake, "na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo." Yani ni juu ya anayemrithi mtoto huyo ikiwa baba hatakuwepo, na mtoto huyo hana mali, basi mrithi wake ni juu yake sawa kile ambacho kiko juu ya baba kama vile kumpa mnyonyeshaji matumizi na mavazi. Kwa hivyo, ikaonyesha ulazima wa jamaa wasio na mali kupewa matumizi na jamaa ambaye ni mrithi mwenye wasaa wa mali. "Na kama wote wawili wakitaka," yani baba na mama "kumwachisha kunyonya." Yani (kumwachisha kunyonya) mtoto huyo kabla ya miaka miwili, "kwa kuridhiana" kwa namna kwamba wote wawili wameridhia. "Na kushauriana," kati yao wawili, je ni kwa masilahi ya mtoto au hapana? Basi ikiwa ni kwa masilahi yake, "basi hakuna ubaya wowote juu yao" katika kumwachisha kunyonya kabla ya miaka miwili. Na Aya pia iliashiria kwa maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba ikiwa mmoja wao ataridhika bila ya mwingineye, au ikiwa siyo kwa masilahi ya mtoto, basi hairuhusiki kumwachisha kunyonya. Na kauli yake, "Na mkitaka kuwapa watoto wenu mama wa kuwanyonyesha." Yani kuwatafutia wanyonyeshaji wasiokuwa mama zao kwa njia isiyokuwa na madhara. "Basi hakuna ubaya juu yenu ikiwa mtapeana mlichoahidi kwa wema". Yani kuwapa hao wanawake wanyonyeshaji "Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda," na atawalipa juu ya hayo kwa mema na mabaya.