پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۲

ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ فِرَٰشًا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءً وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَخْرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا۟ لِلَّهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ۲۲

(22) Na akakuneemesheni kwa neema zilizo dhahiri na zilizofichika. Amekufanyieni ardhi kuwa ni tandiko. Mnakaa sawasawa juu yake, na mnanufaika kwa majengo, kilimo, kulima, na kutembea kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine; na visivyo hivyo miongoni mwa aina za kunufaika nayo. Na akaifanya mbingu kuwa kama mjengo (paa) kwa sababu ya maisha yenu, na akaweka humo manufaa ambayo ni katika mahitaji yenu kama vile jua, mwezi na nyota. "Na akateremsha maji kutoka mbinguni". Na mbingu ni kila kilichoko juu yako, basi hilo ni mbingu. Na kwa sababu hii wafasiri walisema: Kinachokusudiwa hapa na "mbingu" ni mawingu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha maji kutoka humo "na kwayo akatoa mazao" kama vile, nafaka na matunda mfano mitende, mimea na vinginevyo "yawe riziki zenu." Kwavyo mnapata riziki, chakula kikuu, na mnaishi na mnakula matunda. "Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika." Yani wa kumfanana na wenza miongoni mwa viumbe; hivyo mkawaabudu kama mnavyomuabudu Mwenyezi Mungu, na mnawapenda kama mnavyompenda Mwenyezi Mungu, ilhali wao ni kama nyinyi, wameumbwa, wanaruzukiwa na wanaendeshwa. Wao hawamiliki uzito wa chembe katika ardhi wala katika mbingu, wala hawawanufaishi wala hawawadhuru. "Na hali nyinyi mnajua" kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika, wala aliye sawa naye siyo katika kuumba, kuruzuku, na kuendesha mambo, wala katika ibada na ukamilifu. Basi vipi mnaabudu miungu wengine pamoja naye na hali mnajua hilo? Hili ni katika maajabu ya maajabu, na upumbavu wa upumbavu. Na aya hii inajumuisha kati ya amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kukataza kumwabudu asiyekuwa Yeye. Na kubainisha dalili wazi ya ulazima wa kumuabudu Yeye, na ubatili wa kumuabudu asiyekuwa Yeye. Nako ni kutaja Tauhid Ar-rububiyya ambayo inajumuisha kumpwekesha katika uumbaji, kuruzuku na kuendesha mambo. Basi ikiwa kila mtu anakiri kwamba yeye (Mwenyezi Mungu) hana mshirika katika hayo, basi vivyo hivyo naakiri kwamba (Mwenyezi Mungu) hana mshirika katika ibada yake. Na hii ndiyo dalili ya kiakili ya wazi mno juu ya upweke wa Muumba, Mtukufu, na ubatili wa ushirikina. Na kauli yake (Mwenyezi Mungu) "ili mpate kuokoka" inawezekana kuwa maana yake ni kwamba, mkimuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, mtaokoka kwa hilo ghadhabu yake na adhabu yake; kwa sababu mmefanya sababu inayozuia hilo. Na inawezekana kuwa maana yake ni kwamba mkimuabudu Mwenyezi Mungu, mtakuwa miongoni mwa wachamungu ambao wanasifika kwa uchamungu. Na kila ya maana mbili hizi ni sahihi. Nazo (maana mbili hizi) zinaenda sambamba. Kwa sababu, mwenye kufanya ibada kamili; atakuwa miongoni mwa wachamungu. Na atakayekuwa miongoni mwa wachamungu, atapata kuokoka na adhabu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.