Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
سَلْ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ كَمْ ءَاتَيْنَـٰهُم مِّنْ ءَايَةٍۭ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ ۲۱۱
(211) Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu “Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi?” Zinazoashiria haki, na ukweli wa Mitume, na wakawa na yakini nazo na kuzijua, lakini hawakuzishukuru neema hizi ambazo zinahitaji kuzitekeleza. Bali walizikufuru na wakabadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na kwa sababu ya hilo wakastahiki Mwenyezi Mungu kuwateremshia adhabu yake na kuwanyima malipo yake mazuri. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuita kukufuru neema kuwa ni kuzibadalisha. Kwa sababu yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha neema ya kidini au ya kidunia, naye hakuishukuru, na wala hakutimiza wajibu wake, itampungukia na kwenda zake. Na ikabadilishwa na kufuru na maasia, basi kufuru ikawa badala ya neema. Na ama mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na akatekeleza haki yake, basi hiyo (neema) itakaa imara na kuendelea, na Mwenyezi Mungu atamzidishia katika hiyo.