پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۹۶

وَأَتِمُّوا۟ ٱلْحَجَّ وَٱلْعُمْرَةَ لِلَّهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا ٱسْتَيْسَرَ مِنَ ٱلْهَدْىِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا۟ رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ ٱلْهَدْىُ مَحِلَّهُۥ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِۦٓ أَذًى مِّن رَّأْسِهِۦ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَآ أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلْعُمْرَةِ إِلَى ٱلْحَجِّ فَمَا ٱسْتَيْسَرَ مِنَ ٱلْهَدْىِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَـٰثَةِ أَيَّامٍ فِى ٱلْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُۥ حَاضِرِى ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ ۱۹۶

Na Mola Mtukufu alipomaliza [kutaja] hukumu za Saumu na jihadi, akataja hukumu za Hijja, akasema:

{196} Aya hii inatumika kama ushahidi wa kwamba Kauli yake [Mola Mtukufu] “na timizeni Hijja na Umra” inatumika kama dalili ya mambo haya: La kwanza: Ulazima wa kufanya Hija na Umra na ufaradhi wake. La pili: Ulazima wa kuzikamilisha kwa nguzo zake na wajibu zake ambazo ziliashiriwa na kitendo cha Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kauli yake. “Chukueni kutoka kwangu ibada zenu (za Hijja).” La tatu: Kwamba kuna hoja ndani yake kwa yule aliyesema kuwa Umra ni wajibu. La nne: Kwamba Hija na Umra ni lazima zikamilishwe baada ya kuzianza, hata kama ni za sunna. La tano: Amri ya kuzifanya kwa ukamilifu na kwa uzuri. Na hilo ni kiwango cha ziada juu ya kufanya yale yanayowapasa kufanya ndani yake. La sita: Ndani yake kuna amri ya kuzifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. La saba: Kwamba mwenye kuingia katika ihraam ya hayo mawili hawezi kutoki kabisa katika ihraam mpaka atakapozikamilisha. Isipokuwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiondoa katika hiyo hukumu, nacho ni kuzuiwa, ndio maana akasema: “Na ikiwa mtazuiwa,” yani mmezuiwa kuifikia Nyumba ili kuzikamilisha, kwa sababu ya maradhi, au kupotea, au adui, na mfano wa hayo katika aina za kuzuiwa. “Basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana.” Basi chinjeni kilicho chepesi katika dhabihu, ambacho ni subui ya ngamia, au subui ya ng'ombe, au kondoo anayechinjwa na aliyezuiwa. Na anyoe nywele na atoke katika ihramu yake kwa sababu ya kuzuiwa, kama alivyofanya Nabii rehema na amani ziwe juu yake na maswahaba wake, pale washirikina walipowazuia (katika) mwaka wa Al-Hudaybiya. Na asipopata dhabihu, basi afunge badala yake siku kumi kama anavyofanya Al-Mutamatti’ (mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji), kisha atoke katika ihraam. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao.” Na hili ni katika makatazo ya (aliyepo katika) Ihram, yani kuondoa nywele kwa kunyoa au kinginecho kutoka kichwani, au kutoka kwenye mwili, kwa sababu lengo lake ni moja. Kwa sababu, madhumuni ya hilo ni kuwa na nywele timutimu na kuzuia kupata raha ya kuiondoa, na hilo linapatikana pia katika nywele nyinginezo. Na wanachuoni wengi walilinganisha kukata kucha na uondoaji wa nywele kwa sababu ya starehe inayopatikana ndani ya mawili hayo. Na katazo hilo la hayo yaliyotajwa linaendelea mpaka mnyama huyo afike machinjoni mwake. Nayo ni siku ya An-Nahr. Na ni bora zaidi kunyoa kuwe baada ya kuchinja, kama Aya inavyoashiria hilo. Aya hii inatumika kama dalili ya kwamba Al-Mutamatti’, (mtu anayejistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndiyo akahiji), anapomleta dhabihu haruhusiwi kutoka katika ihram ya Umra yake kabla ya siku ya An-Nahr (Siku ya kuchinja). Na anapoizunguka Al-Kaa’ba na akafanya Saa'yi ya Umra, anaingia katika Ihram ya Hija, na hawezi kutoka katika Ihram kwa sababu ya kumleta dhabihu huyo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikataza hilo kwa sababu ya yale yaliyomo katika hilo ya unyenyekevu na utiifu kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. Na kuvunjika kwa sababu yake, na kujiweka chini sana kwa sababu yake, ambako ndiko masilahi ya mja yenyewe, ikiwa hakuna ubaya wowote juu yake katika hilo. Lakini yakitokea madhara yoyote kama vile akiwa na maudhi kutokana na maradhi ambayo kwa kunyoa kichwa chake atanufaika kwa hilo, au vidonda, au chawa na mfano wa hayo. Basi anaruhusiwa kunyoa kichwa chake, lakini inamlazimu atoe fidia ya kufunga saumu siku tatu, au kuwapa masikini sita sadaka, au kuchinja kile kinachotosheleza katika udh-hiya (dhabihu wanochinjwa siku ya Iddi). Naye amepewa chaguo, lakini kuchinja ni bora zaidi, kisha sadaka, kisha kufunga saumu. Na mfano wa hivyo ni kila kitu chenye maana hiyo kama vile kukata kucha, au kufunika kichwa, au kuvaa nguo zilizoshonwa, au manukato. Haya yote yanaruhusiwa wakati wa dharura, pamoja na ulazima wa kutoa fidia iliyotajwa hapo awali, kwa sababu makusudio ya hayo yote ni kuondoa kila ambacho anastareheka kwacho. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Na mtakapokuwa na amani,” yani mnaweza kuifikia Nyumba ya Al-Ka’ba bila ya kuzuiwa na adui na mfano wake. “Basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndiyo akahiji” kwa kuitumia kama njia ya kuifikia (Hijja) kwa kufaidika katika kustarehe baada ya kuikamilisha (yani Umra). "Basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata.” Yani inamlazimu chochote ambacho ni chepesi kwake katika dhabihu. Naye ni yule anayetosheleza katika Udh-hiya. Na hii ndiyo damu ya dhabihu ya ibada kwa sababu ya kuweza kufanya ibada hizo mbili katika safari moja. Na kwa sababu ya neema ambayo Mwenyezi Mungu amempa ya kujistarehesha baada ya kumaliza Umra, na kabla ya kuanza Hijja. Na mfano wa hilo ni Al-Qir-an (mtu anayefanya Umra kwa kuiingiza ndani ya Hija) kwa sababu ya kufanya ibada hizo mbili kwa pamoja. Na maana ya Aya hii isiyo ya moja kwa moja inaashiria kuwa mwenye kufanya Hijja peke yake halazimiki kutoa dhabihu. Na Aya hii pia inaashiria kuruhusiwa, bali ni fadhila ya kujistarehesha baada ya kumaliza Umra, na kuruhusika kuifanya (Umra) katika miezi ya Hijja. “Na asiyepata,” yani dhabihu au bei yake, “afunge siku tatu katika Hijja.” Ambayo inaruhusika kuanzia wakati wa kuingia katika Ihraam ya Umra, na mwisho wake ni siku tatu baada ya kuchinja, zile siku za kupiga vijiwe kwenye Al-Jamaraat, na kulala usiku huko Mina. Lakini lililo bora zaidi katika hizo ni kwamba afunge (siku) ya saba, na ya nane, na ya tisa. “Na siku saba mtakaporudi,” yani mtakapokuwa mmemaliza matendo ya Hijja. Kwa hivyo, inaruhusika kufanya hivyo huko Makka, na njiani, na baada ya kuwasili kwake kwa watu wake. “Hayo,” yaliyotajwa ya uwajibu wa kutoa dhabihu kwa Al-Mutamtti’ “ni kwa yule ambaye jamaa zake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu.” Ikiwa yuko kwenye umbali wa kufupisha swala au zaidi, au mbali zaidi kulingana na ada. Na huyu ndiye anayewajibika kutoa dhabihu, kwa sababu aliweza kufanya ibada hizo mbili katika safari moja. Na ama yule ambaye jamaa zake wako karibu na Msikiti Mtakatifu, basi halazimiki kutoa dhabihu kwa sababu ya kutokuwepo lenye kulazimisha hilo. “Na mcheni Mwenyezi Mungu.” Yani katika mambo yenu yote kwa kufuata maamrisho yake na kujiepusha makatazo yake. Na katika hayo ni kufuata kwenu maamrisho haya, na kujiepusha na makatazo haya yaliyotajwa katika Aya hii. “Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu,” yani mwenye kumuasi. Na hili ndilo lenye kuleta uchamungu. Kwa sababu, mwenye kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu, atajiepusha na yenye kusababisha adhabu. Kama vile mwenye kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu, atafanya yenye kumfikisha kwenye malipo. Na ama yule ambaye haogopi adhabu, wala hatarajii malipo, hujiingiza ndani ya yale yaliyoharamishwa na akajasiri kuwacha yale ya wajibu.