Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِىَ مَوَٰقِيتُ لِلنَّاسِ وَٱلْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ ٱلْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا۟ ٱلْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ ٱلْبِرَّ مَنِ ٱتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا۟ ٱلْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَٰبِهَا ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۱۸۹
{189} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi.” Ahilla ni wingi wa hilaal (miezi miandamo). Ni nini faida yake na hekima yake? Au yenyewe ni nini? “Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu“. Yani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliifanya kutokana na wema wake na rehema juu yake kwa huu mpangilio. Miezi miandamo inazunguka ikiwa dhaifu katika mwanzo wa mwezi, kisha inongezeka hadi nusu yake, kisha inaanza kupunguka mpaka iishe. Na vivyo hivyo, ili watu wajue kwa hilo nyakati za ibada zao kama vile kufunga Saumu, na nyakati za Zaka, na kafara mbalimbali, na nyakati za Hija. Na kwa kuwa Hija hufanyika katika miezi inayojulikana, na inachukua muda mwingi, akasema: “Na Hija.” Na pia hujulikana kwayo madeni yaliyoahirishwa, na muda wa kodi, na muda wa eda na mimba, na yasiyokuwa hayo katika yale ambayo ni katika mahitaji ya viumbe. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifanya kuwa ni hesabu ambayo kila mtu anaijua, kuanzia mdogo na mkubwa, wenye elimu na wasiokuwa na elimu (wajinga). Na ikiwa hesabu ingekuwa kwa mwaka wa jua, basi hawangeijua isipokuwa wachache tu miongoni mwa watu. “Wala sio wema kwamba mziingie nyumba kwa nyuma yake.” Hili ni kama vile walivyokuwa Ansari na Waarabu wengine walipokuwa wanaingia kwenye Ihram. Hawakuwa wanaziingia nyumba kupitia milangoni mwake wakiifanya hiyo kuwa ibada, na wakidhani kuwa ni wema. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akatoa habari kwamba sio wema, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwawekea sheria hiyo. Na kila mwenye kuabudu kwa ibada ambayo Mwenyezi Mungu hakuifanya kuwa sheria wala Mtume wake, basi yeye anafanya bidaa kuwa ibada. Na Mwenyezi Mungu akawaamrisha kwamba waingie majumbani kupitia milangoni mwake, kwa sababu ya urahisi uliopo katika hilo kwao; ambao (huo urahisi) ni mojawapo ya misingi ya sheria. Na inafahamika kutokana na dalili ya Aya hii kuwa katika kila jambo miongoni mwa mambo, mtu anafaa kulijia kwa upande wake mwepesi ulio karibu. Ambao Mwenyezi Mungu ameufanya kuwa njia ya kulifikia. Kwa hivyo, mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu, anafaa kuangalia katika hali ya yule aliyeamrishwa. Na atumie upole na sera nzuri pamoja naye, ambazo kwazo yote au baadhi ya makusudio yanafikiwa. Na mwanafunzi na mwalimu wanafaa kuchukua njia ya karibu na nyepesi zaidi ambayo lengo lake linafikiwa kwayo. Na vivyo hivyo, kila anayejaribu jambo miongoni mwa mambo, na akalijia kutoka kwenye milango yake, na akavumilia juu yake, basi hakuna budi atapata makusudio yake kwa msaada wa Mfalme Anayeabudiwa. “Na mcheni Mwenyezi Mungu.” Huu ndio wema ambao Mwenyezi Mungu aliamrisha, ambao ni kushikana na kumcha Yeye daima, kwa kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake. Kwani hilo ndiyo sababu ya kufaulu, ambako ndiko kupata yale yanayotafutwa, na kuokoka kutokana na yanayohofiwa. Kwa hivyo, mwenye kutomcha Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hatakuwa na njia ya kufaulu. Na mwenye kumcha, atapata kufaulu na kupita.