Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ نَزَّلَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ ۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِى ٱلْكِتَـٰبِ لَفِى شِقَاقٍۭ بَعِيدٍ ۱۷۶
(176) “Hayo,” yaliyotajwa ambayo ni malipo yake kwa uadilifu, na kuzuia kwake sababu za uwongofu kwa yule aliyezikataa na akachagua zisizokuwa hizo. “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki.” Na katika haki ni kumlipa mwema kwa wema wake, na mwovu kwa wovu wake. Na pia katika kauli yake, “ameteremsha Kitabu kwa haki;” kuna dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu alikiteremsha ili kuwaongoa viumbe wake, na kubainisha haki kutokana na batili. Kwa hivyo, mwenye kukigeuza kutoka kwa makusudio yake, basi yeye anastahiki kulipwa kwa adhabu kubwa kabisa. “Na hakika, wale waliohitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki.” Yani kwa hakika wale waliohitalifiana katika Kitabu, na wakaamini baadhi yake na baadhi yake wakaikataa, na wale waliokibadilisha na wakakigeuza kwa matamanio yao na malengo yao. “Wamo katika upinzani ulio mbali na haki” kwa sababu walikihalifu Kitabu kilicholeta haki yenye kuleta kuafikiana na kutopingana. Basi mambo yao yakachafuka, na upinzani wao ukawa mwingi, na hilo likasababisha kujitenga kwao, kinyume na Ahlul-Kitab (watu wa Kitabu). Ambao walikiamini na wakahukumu kwacho katika kila jambo, hao walikubaliana na wakafanya urafiki kwa mapenzi na umoja juu yake. Aya hizi zilijumuisha tishio kwa wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Wanaopendelea badala yake mapambo ya dunia kwa adhabu na ghadhabu, na kwamba Mwenyezi Mungu hatawatakasa kwa kuwawezesha wala kwa msamaha. Na akataja sababu ya hayo, kwamba ni kupendelea kwao upotovu kuliko uwongofu, na hilo likapelekea kuchagua adhabu kuliko msamaha. Kisha akawaonea uchungu katika ukubwa wa subira yao juu ya moto, kwa sababu ya kutenda kwao sababu ambazo wanajua kuwa zinafikisha huko. Na kwamba Kitabu hiki kinajumuisha haki inayolazimu mapatano juu yake, na kutotengana. Na kwamba kila anayekipinga yuko mbali sana na haki, na kwamba yuko katika mzozo na ugomvi, na Mwenyzi Mungu anajua zaidi.