پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۷۳

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيْرِ ٱللَّهِ ۖ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ۱۷۳

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuruhusiwa kwa vilivyo vizuri, akataja uharamu wa vilivyo vichafu, akasema: “Yeye amekuharimishieni mzoga tu.” Nao ni kilichokufa bila ya kuchinjwa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Kwa sababu, mzoga ni mchafu na una madhara, kutokana na ubaya wake wenyewe na kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kuwa; kufa kwake kulitokana na maradhi, hivyo ukaongeza madhara. Na Mwenye Sheria ya Kiislamu aliwatenga kutoka kwa ujumla huu nzige waliokufa na samaki wa baharini, kwa kuwa ni halali na wazuri. “Na damu” yani Al-Masfuuh (inayotoka kwa wingi), kama ilivyozuiliwa hivi katika Aya zinginezo. “Na kilichotajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika kuchinjwa kwake.” Yani kilichinjwa kwa sababu ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kama vile wale wanaochinjwa kwa sababu ya masanamu na Awthaan (chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu, kinachoabudiwa huku kimeridhia). Kama vile mawe, makaburi na mfano wake. Na haya yaliyotajwa hapa hayafungii vilivyo haramu katika hivi tu, lakini vilitajwa ili kubainisha aina za machafu yaliyoashiriwa katika maana ya kauli yake “vizuri”. Kwa hivyo, jumla ya vile vilivyoharamishwa inapatikana kutoka katika Aya iliyotangulia kutoka kwa kauli yake, “halali na vizuri,” kama ilivyotangulia. Na alituharamishia vitu hivi vichafu na mfano wake kwa kutufanyia upole, na kutuepusha na madhara. Na pamoja na hili; “lakini aliyefikiwa na dharura.” Yani aliyelazimika kutumia kilicho haramu kwa sababu ya njaa na ukosefu, au kulazimishwa “bila ya kutamani.” Yani bila kuitafuta hiyo haramu huku anao uwezo wa kutumia kilicho halali, au bila yeye kuwa na njaa. "Wala kupita kiasi,” yani kupita mpaka katika kula kile alichoruhusiwa kwa sababu ya dharura. Basi mwenye kulazimishwa na hali hawezi kupata kilicho halali, na akala kadiri ya dharura hiyo, basi asizidishe juu yake. “Basi yeye hana dhambi” [yani ubaya] juu yake. Na ikiwa ubaya na dhambi vitakwisha, bali hilo jambo (la uharamu) litarejea jinsi lilivyokuwa. Na mtu aliye katika hali hii ameamrishwa ale, bali ni amekatazwa kujitupa kwa mkono wake katika maangamizo, na kuiua nafsi yake. Kwa hivyo, inalazimu ale, na anapata dhambi ikiwa ataacha kula mpaka akafa; ambapo atakuwa ameiua nafsi yake. Na ruhusa hii na ukunjufu ni kunatokana na rehema yake, Aliyetukuka kwa waja wake. Na ndiyo maana akaihitimisha (Aya hii) kwa majina haya yake mawili matukufu, yanayofaa kufaa kukubwa zaidi, akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”. Na kwa vile uhalali uliwekewa masharti haya mawili, na akawa mtu aliye katika hali hii kuenda asichunguze kwa ukamilifu; - Mola Mtukufu akasema kuwa Yeye ni Mwenye kusamehe.- Hivyo husamehe alichokosea katika hali hii, hasa kwa sababu alishindwa na dharura hiyo, na ugumu ukaondoka hisia zake. Na katika Aya hii, kuna dalili ya kanuni inayojulikana sana ambayo ni, “dharura (mahitaji) hufanya yaliyokatazwa kuruhusika.” Hivyo, kila jambo lililokatazwa ambalo mtu analazimishwa juu yake, basi amekwisharuhusiwa na Mfalme, Mwingi wa Rehema. [Basi ni zake sifa njema zote na shukrani, mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na ndani].