پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۴۵

وَلَئِنْ أَتَيْتَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ بِكُلِّ ءَايَةٍ مَّا تَبِعُوا۟ قِبْلَتَكَ ۚ وَمَآ أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعْتَ أَهْوَآءَهُم مِّنۢ بَعْدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۱۴۵

(145) Alikuwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kutokana na ukamilifu wa pupa yake ya kuwaongoza viumbe, akiwapa [wao] nasaha nyingi namna awezavyo. Na anafanya upole katika kuwaongoza, na anahuzunika wasipoifuata amri ya Mwenyezi Mungu. Basi miongoni mwa makafiri kulikuwa yule aliyeasi amri ya Mwenyezi Mungu na akawafanyia kiburi Mitume wa Mwenyezi Mungu, na akaacha uwongofu kwa makusudi na kwa uadui. Na miongoni mwao ni Mayahudi na Wakristo, watu wa Kitabu cha kwanza ambao walimkufuru Muhammad baada ya kuwa na yakini, na si kwa ujinga. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia kwamba, wewe “hata ukiwaletea hao waliopewa Kitabu hoja za kila namna.” Yani kwa kila ushahidi na dalili inayobainisha kauli yako na inayobainisha unayolingania; “hawatafuata Kibla chako,” yani hawatakufuata. Kwa sababu, kufuata kibla ni dalili ya kumfuata (Mtume), na kwa kuwa sababu ni suala la kibla. Na jambo hili lilikuwa hivyo kwa sababu wao ni wakaidi walioijua haki na wakaiacha. Hivyo basi, aya (hoja) [zinamfaidisha na] ananufaika nazo anayeifuata haki hali ya kuwa haiko wazi kwake; kwa hivyo, zinambainishia Aya hizo wazi. Na ama mwenye kuweka azma ya kutofuata haki, basi huyo hana hila. Na pia imeshatokea hitilafu baina yao, na baadhi yao hawafuati kibla ya wengine. Kwa hivyo, hilo si ajabu kwao, pamoja na hayo wao kutofuata kibla chako, ewe Muhammad, na wao ndio maadui wa kweli, wenye husuda. Na kauli yake: “Wala wewe hutafuata kibla chao,” ni yenye ufasaha kuliko kauli yake ‘wala usifuate.’ Kwa sababu, hiyo ina maana kwamba yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa na sifa ya kuwapinga, hivyo basi haiwezekani kutokea hilo kutoka kwake. Na wala hakusema kwamba ‘hata wakipewa kila Aya’ kwa sababu hawana ushahidi kwa kauli yao. Na pia ikiwa ukweli utabainika kwa dalili zake za yakini, si lazima kuleta majibu ya fikira potofu zinazozijia, kwa sababu hazina kikomo. Na kwa sababu unajulikana ubatili wake kuwa inajulikana kwamba chochote chenye kupingana na ukweli ulio wazi, hicho ni batili. Kwa hivyo, linakuwa suluhisho la hizo fikira potofu ni katika mlango wa kujitolea. “Na kama ukiyafuata matamanio yao,” Yeye alisema tu ‘matamanio yao’ na wala hakusema ‘dini yao’. Kwa sababu yale waliyoko juu yake ni matamanio ya nafsi tu, hata wao wanajua nyoyoni mwao kuwa hiyo si dini. Na mwenye kuacha dini yake, atafuata matamanio, na hakuna shaka. Mola Mtukufu alisema: “Je, umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake?” (Na akasema,) “baada ya kile kilichokufikia katika elimu,” kwamba wewe uko katika haki, nao wako katika batili; “wewe kwa hakika hapo,” yani ukiwafuata. Na huku ni kuondoa ili sentensi hii isije ikatengana na ile ya kabla yake hata ikiwa ni katika ufahamu, “utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.” Yani ndani yao na kujumuishwa katika hukumu yao. Na ni dhuluma gani kubwa kuliko dhuluma ya aliyeijua haki na batili? Kisha akaipendelea batili juu ya haki. Na hili hata kama anaambiwa yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – maneno haya, umma wake umejumuishwa katika hayo. Na pia lau kuwa yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - angefanya hivyo - Mwenyezi Mungu amwepushie hilo, - utakuwa udhalimu licha ya cheo chake cha juu na wingi wa wema wake. Basi asiyekuwa yeye ndiye anayefaa zaidi (kutofuata). Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: