Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطَ كَانُوا۟ هُودًا أَوْ نَصَـٰرَىٰ ۗ قُلْ ءَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ ٱللَّهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَـٰدَةً عِندَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ۱۴۰
(140) Na haya ni madai mengine kutoka kwao, na kuhojiana katika Mitume wa Mwenyezi Mungu. Walidai kuwa wao wanawastahiki zaidi Mitume hawa waliotajwa kuliko Waislamu. Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema: "Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?" Mwenyezi Mungu anasema, "Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina." Nao wanasema, bali yeye alikuwa ni Myahudi au Mkristo. Basi ima hao ndio wakweli na wenye elimu (la hilo), au Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mkweli na mwenye elimu ya hilo. Kwa maana, moja ya hayo mambo mawili ni hakika na hakuna njia nyingine. Na sura ya jibu siyo bayana. Lakini liko wazi na bainifu kabisa, kiasi kwamba kutokana na uwazi wake hakuhitaji kusema kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ajuae zaidi, naye ndiye mkweli zaidi, na mfano wake, kwa sababu liko wazi kwa kila mtu. Ni kama ingesemwa: Usiku ndio unaangaza zaidi au mchana? Na mchana ndio moto zaidi au maji? Na je , ushirikina ndio bora au Tauhid? na mfano wa hayo. Na haya anayajua kila mwenye akili hata kidogo kiasi kwamba wao wenyewe wanalijua hilo, na wanajua kwamba Ibrahim na Mitume wengine hawakuwa Mayahudi wala Wakristo, kwa hivyo wakaificha elimu hii na ushahidi huu. Na kwa sababu ya hayo, dhuluma yao ilikuwa kubwa zaidi. Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu?" Na ni ushahidi walio nao uliowekwa kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu, siyo kutoka kwa viumbe. Kwa hivyo, inahitaji kufanya hima kuisimamisha, lakini wao wakaificha na wakadhihirisha kinyume chake. Wakakusanya kati ya kuficha haki na kutoitamka, na kuonyesha uwongo na kuulingania. Je, hii si dhuluma kubwa zaidi? Ndiyo. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, na atawaadhibu juu yake kwa adhabu kali kabisa. Ndio maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo." Bali alikwishathibiti vitendo vyao na akavihisabu, na akawahifadhia ujira wake. Basi malipo mabaya zaidi ni malipo yao, na Moto ndio makazi maovu mno ya madhalimu. Na hii ndiyo njia ya Qur-ani katika kutaja elimu na uwezo (wa Mwenyezi Mungu) nyuma ya Aya zilizomo matendo ambayo yanaadhibiwa juu yake. Basi hilo linamaanisha ahadi, maonyo, vitisho na kuhofisha. Na pia kutaja Majina mazuri (ya Mwenyezi Mungu) baada ya hukumu inamaanisha kwamba, amri ya kidini na ya kiadhabu ni athari katika athari zake, na yenye kuleta miongoni mwa vyenye kuleta vyake; na kwamba yanalazimu hivyo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: