Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلِلَّهِ ٱلْمَشْرِقُ وَٱلْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا۟ فَثَمَّ وَجْهُ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ ۱۱۵
(115) Yani "Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu." na alizitaja hususan kwa sababu hizo ndizo mahali pa ishara kubwa [kwani mbili hizo ndizo] mapambazuko ya mianga na magharibi yake. Basi ikiwa yeye ndiye mmiliki wake, yeye ndiye mmiliki wa pande zote. "Basi kokote mnakoelekea," nyuso zenu miongoni mwa pande, ikiwa kuzielekea kwenu ni kwa amri yake; ima anakuamrisheni kuielekea Al-Kaaba baada ya kuamrishwa kuielekea Al-Bait Al-Maqdis, au mmeamrishwa kuswali katika safiri juu ya ngamia na mfano wake; basi Qibla ni popote anapoelekeza mja. Au ikiwa Qibla kinakuwa na mashaka, basi atajaribu kuswali kwa kukielekea, kisha hilo kosa likimdhihirikia au awe ni mwenye udhuru kwa sababu ya kusulubiwa au maradhi na mfano wake, basi katika haya mambo, mja huwa amepewa udhuru au ameamrishwa. Vyovyote iwavyo, kuelekea upande miongoni mwa pande hakutoki nje ya milki ya Mola wake Mlezi, "uso wa Mwenyezi Mungu upo (upande huo). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkunjufu) na Mwenye elimu." Ndani yake kuna kumthibitishia Mwenyezi Mungu uso kwa namna inayomfaa Yeye Mtukufu. Na kwamba Mwenyezi Mungu ana uso usiofanana na nyuso zingine. Naye Mtukufu (Mwenyezi Mungu) ni mkunjufu (mpana) wa fadhila, na sifa nyingi kuu, Mjuzi wa siri na makusudio yenu. Na katika wasaa wake na elimu yake, ni kwamba aliwafanyia ukunjufu katika jambo hili, na akakubali kutoka kwenu alilowaamrisha. Basi ni zake sifa njema na shukrani.