Maryam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَىَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُۥٓ ءَايَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا ۲۱
{21} "(Malaika) akasema: Hivyo ndiyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu," inayoonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwamba sababu zote haziathiri zenyewe tu, lakini huathiri kwa Mwenyezi Mungu kuzifanya ziathiri. Kwa hivyo Yeye huwaonyesha waja wake ukiukaji wa ada ya kawaida kuhusiana na sababu fulani za kawaida, ili wasisimamie tu kwenye sababu hizo, na wakakosa kumuangalia yule aliyeziweka na anayezisababisha. "Na" ili tumfanye kuwa yeye na kuzaliwa kwake" ni rehema kutoka kwetu" kwake, na kwa mama yake, na kwa watu. Ama rehema ya Mwenyezi Mungu kwake, ni kule kumteua Mwenyezi Mungu kwa kumpa ufunuo wake, na akamneemesha kwa yale aliyowaneemesha kwayo Mitume wenye stahamala kubwa. Na ama rehema yake kwa mama yake, ni ile fahari aliyopata na sifa nzuri, na manufaa makubwa. Na ama rehema yake kwa watu, ni kwamba neema yake kubwa juu yao ni kwamba aliwatumia Mtume miongoni mwao anayewasomea Aya zake, na kuwatakasa, na kuwafundisha Kitabu na hekima, ili wamuamini, na wamtii, na wapate furaha ya dunia na akhera. Na kupatikana kwa Isa kwa njia hii "lilikuwa jambo liliokwisha hukumiwa" kitambo na halikuwa budi kutokea. Kwa hivyo Jibril, amani iwe juu yake, akapuliza katika nafasi ya kuingilia kichwa kwenye nguo.