پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
سورهٔ ۱۸

Al-Kahf

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۰

إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِى مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا ۲۰

{20} Na wakataja yale yanayotahadhariwa katika wengine kuwajua na wao kuwadhihirikia wengine nayo ni kuwa wao wako baina ya vitu viwili: ima kupigwa mawe na kuwaua mauaji mabaya zaidi kwa sababu ya kuwaghadhibikia wao na dini yao, au kuwatia katika majaribio ili waiache Dini yao na kuwarejesha katika mila zao. Na katika hali hii hawatafaulu kamwe, bali watapata hasara katika Dini yao, dunia yao na Akhera yao. Na Aya hizi mbili ziliashiria manufaa kadhaa: Miongoni mwake ni kuhimiza kutafuta elimu na kuifanyia utafiti elimu hiyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwainua kutoka usingizini kwa ajili ya hayo. Na miongoni mwake ni kwamba adabu njema kwa yule ambaye amechanganyikiwa katika elimu yake ni kuirejesha kwa anayeijua, na kwamba asimamie kwenye kikomo chake. Na miongoni mwake ni kwamba kuwakilisha wengine kunaruhusika katika kuuza na kununua na kwamba kufanya ushirika katika hayo kunaruhusika. Na miongoni mwake ni kwamba inaruhusika kula vitu vizuri na vyakula vitamu ikiwa havijafikia kiwango cha kupitiliza mipaka ambako kulikatazwa, kwa sababu ya kauli yake, "akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula" hasa ikiwa mtu huyo haimfailii kitu kingine isipokuwa hicho. Na huenda huu ndio msingi wa wafasiri wengi wanaosema kuwa hawa ni watoto wa wafalme. Kwa sababu walimwamuru aje na vyakula bora zaidi ambavyo kwa kawaida watu matajiri huvila. Na miongoni mwake ni kuhimiza kutahadhari, kujificha, na kujiweka mbali na maeneo ya majaribio katika dini, na kutumia usiri katika kumficha mtu na ndugu zake katika dini. N miongoni mwake ni kwamba utashi mkubwa mno wa vijana hao juu ya dini, na kukimbia kwao kila majaribio katika dini yao, na kuziacha nchi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni kwamba kutaja madhara na uharibifu uliomo ndani ya uovu yanayomfanya mtu kuuchukia na kuuacha, na kwamba njia hii ndiyo njia ya Waumini wa mwanzo na wa baadaye, kama wanavyosema, “Na hapo hamtafaulu kamwe."