پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
سورهٔ ۱۷

Al-Israa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۶۰

وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِٱلنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا ٱلرُّءْيَا ٱلَّتِىٓ أَرَيْنَـٰكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَٱلشَّجَرَةَ ٱلْمَلْعُونَةَ فِى ٱلْقُرْءَانِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَـٰنًا كَبِيرًا ۶۰

{60} "Na tulipokwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu" kwa elimu na uwezo. Hawana kimbilio la kukimbilia kutoka kwake. Na hili linamtosha mwenye akili kuachana na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu ambaye amewazunguka watu. "Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha" wengi wa wafasiri wanaona kuwa ni usiku wa Safari ya Al-Isra, "na mti ule uliolaaniwa" ambao ulitajwa "katika Qur-ani" nao ni mti wa Zakumu unaotoka katikati ya Jahim. Maana yake ni kwamba ikiwa mambo haya mawili yamekuwa ni fitna kwa watu, hata makafiri wakawa na ujasiri wa kufanya ukafiri wao na uovu wao ukaongezeka, na baadhi ya wale ambao imani yao ilikuwa dhaifu wakatoka katika imani yao, kwa sababu ya yale aliyowaambia kuhusu mambo yaliyotokea usiku wa Safari ya Al-Isra, na kusafiri kwake usiku kutoka Msikiti Mtukufu hadi Msikiti wa Al-Aqsa, hayakuwa ya kawaida. Na kujulisha kwake pia kwamba kuna mti unaoota katikati ya Moto wa Jahiim kulikuwa jambo lisilo la kawaida. Basi hayo ndiyo yaliyowafanya kukadhibisha. Basi ingekuwaje ikiwa wangeona ishara kubwa kubwa na miujiza mikubwa? Je, hayo si uwezekano mkubwa wa kwamba wataongeza uovu wao kwa sababu yake? Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawarehemu na akawaondolea hayo. Na kwa sababu ya hili, utajua kwamba kutotaja kwa uwazi katika Qur-ani na Sunnah mambo makubwa yaliyotokea siku zama za mwisho ni bora zaidi. Kwa sababu mambo ambayo watu hawajawahi kushuhudia mfano wake huenda yasikubaliwe na akili zao, [kama wangeambiwa hayo kabla ya kutokea kwake], na yakatia shaka katika nyoyo za baadhi ya waumini na kizuizi kinachozuia yule ambaye hajaingia katika Uislamu na kumfanya kujitenga mbali na Uislamu. Badala yake, Mwenyezi Mungu alitaja maneno ya jumla yenye kujumuisha kila kitu kitakachokuwepo. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. "Na tunawahofisha" kwa ishara mbalimbali "lakini haiwazidishii" hiyo hofu "isipokuwa uasi mkubwa." Na hali hii ndiyo mbaya zaidi ya kufanya uovu na kuupenda, na kuichukia heri na kutoifuata.