An-Nahl
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّتِى نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنۢ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَـٰثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَـٰنَكُمْ دَخَلًۢا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِىَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ۹۲
{92} "Wala msiwe," katika kuvunja kwenu maagano kwa mithali mbaya na mbaya kabisa na ushahidi wa upumbavu wa wale wanaozitumia. Ambao ni "kama mwanamke yule" anayeusokota uzi wake ukawa mgumu, na pindi unapokuwa imara na ukatimia kama ulivyotakiwa kuwa, anaufumua na kuufanya kuwa, "umezongoka." Basi akawa alitaabisha kuusokota, tena akataabika katika kuufumua na wala hakufaidika isipokuwa kuambulia patupu, taabu, upumbavu wa kiakili, na upungufu wa kimaoni. Basi hivyo ndivyo alivyo mwenye kuvunja agano lake. Anakuwa dhalimu, mjinga, mpumbavu, mpungufu wa dini, na uungwana. Na kauli yake, "Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine?" Yaani, hali hii haiwafailii, kwamba mfunge viapo vya mkazo, kisha mkangojea fursa, ikiwa aliyevifunga ni dhaifu, asiyemuweza mwenzake huyo, anavitimiza siyo kwa sababu ya kuutukuza mkataba na kiapo hicho, lakini kwa sababu ya kutoweza kwake kuuvunjilia mbali. Na ikiwa ina nguvu, na anaona kwamba kuna masilahi ya kidunia katika kuuvunja, anauvunja bila ya kujali agano na kiapo cha Mwenyezi Mungu. Na hayo yote yanakuwa kulingana na matamanio ya nafsi roho na kuyatanguliza mbele ya makusudio ya Mwenyezi Mungu kwenu, na kuyatanguliza pia mbele ya uungwana wa kibinadamu na tabia zinazoridhiwa, kwa sababu tu kwamba umma mmoja ni wengi na wenye nguvu zaidi ya wenzao. Haya ni majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtihani ambao [Mwenyezi Mungu] anawajaribu kwa huo, kwani aliweka sababu za kuwajaribia ambazo anamjaribu kwazo mkweli atimizaye kutokana na muovu mwana mashaka. "Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Qiyama yale mliyokuwa mkikhitalifiana ndani yake." Kisha atamlipa kila mmoja kwa matendo yake, na atawahizi waliovunja ahadi zao.